Pata taarifa kuu
UN-CORONA-AFYA

Covid-19: Mapigano yasitishwa katika nchi kadhaa duniani, Umoja wa Mataifa wapongeza

Umoja wa Mataifa umekaribisha tangazo la kusitisha mapigano katika nchi kadhaa zilizokuwa zikikumbwa na vita, baada ya wito wake wa kusitisha mapigano kufuatia mripuko wa ugonjwa wa Covid-19.

Vita katika nchi nyingi duniani vimeua watu wengi.
Vita katika nchi nyingi duniani vimeua watu wengi. Bakr ALKASEM / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inaelekea kuungwa mkono na maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Mkutano Mkuu wa umoja huo.

Hatua ya kusitishwa mapigano ilitangazwa hivi karibuni nchini Ufilipino, Cameroon, Yemen na Syria.

Siku ya Jumatatu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres alitoa wito "wa kusitisha mapigano, " ili kuwalinda raia walio hatarini zaidi katika nchi zenye migogoro dhidi ya janga la Covid-19.

Kwa mujibu wa mwanadiplomasia mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe, "rasimu ya azimio hilo ilizunguka kati ya wanachama watano wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusiana na athari za ugonjwa wa Covid-19 juu ya hali ya amani na usalama kwenye ajenda ya kikao cha Baraza la Usalama"

"Baadhi ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zinafikiria kuunga mkono wito wa Guterres," chanzo kingine cha kidiplomasia kimethibitisha.

Kulingana na vyanzo rasmi, Ufaransa ndio iliandaa mpango huo. Usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alizungumza kwenye mtandao wa Twitter juu ya kuandaa "mpango mpya muhimu" kukabiliana na janga hilo, baada ya mazungumzo na mwenzake wa Marekani, Donald Trump.

Haijajulikana ikiwa mpango huo una uhusiano wowote na rasimu ya azimio iliyojadiliwa na Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.