Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-CORONA-AFYA

Zimbabwe: Wauguzi walalamikia ukosefu wa maandalizi kwa kitisho cha Covid-19

Ugonjwa wa Covid-19 umeendelea kuwa gumzo na kitisho kwa nchi za Kusini mwa Afrika ambazo hazijaathirika na ugonjwa huo, hususan Zimbabwe. Zimbabwe ambayo ni jirani na Afrika Kusini ambayo ina visa vya maambukizi zaidi ya 100, haijafunga mipaka yake na nchi hiyo.

mmoja wa wauguzi akiosha mikono katika hospitali huko Harare, Zimbabwe, Machi 11, 2020.
mmoja wa wauguzi akiosha mikono katika hospitali huko Harare, Zimbabwe, Machi 11, 2020. REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo Jumatatu wiki hii rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, alitangaza janga la asili kufuatia mlipuko wa janga la Corona. Lakini mipaka inaendelea kuwa wazi, hali ambayo imezua wasiwasi mwingi kwa sababu Afrika Kusini, ambayo ni jirani ya Zimbabwe, tayari ina visa vya maambukizi zaidi ya 100 vilivothibitishwa.

Mpaka sasa nchini Zimbabwe hakujaripotiwa kesi yoyote ya maambukizi. Lakini rais Mnangagwa amepiga marufuku sherehe kadhaa, ikiwa ni pamoja na maadhimisho ya uhuru, ambayo yalikuwa yamepangwa kufanyika mwezi ujao.

Kwa sababu ni suala la muda kabla ya ugonjwa huo kuibuka nchini Zimbabwe, daktari mmoja anayehudumu katika moja ya hospitali ya mjini Harare, ambaye hakutaja jina lake, amesema.

"Hatuko tayari, tunakabiliwa na ukosefu wa kila kitu, wafanyakazi, dawa na vifaa, "daktari huyo ameaongeza.

"Katika hospitali ambapo ninafanyia kazi, tuna mask 300 tu ambazo zinatakiwa kutumiwa katika hospitali nzima. Hatuna vifaa vya kutulinda. Na katika wodi ya wagonjwa mahututi kuna vitanda vitatu tu, ambavyo tayari vina wagonjwa. Mamlaka inasema "osheni mikono", lakini hakuna maji. Ikiwa utaletwa hapa katika hali mahututi, utaaga dunia mapema, kwa sababu hatuna vifaa vya kutibu, "amebaini.

Madaktari wanakubaliana na mfumo huu wa afya ambao umekuwa ulishindwa kwa miaka kadhaa: kipaumbele ni kuzuia. Na haswa kuzuia virusi kuenea, amesema daktari mwengine ambaye hakutaka kutaja jina lake.

"Kuwepo tu na ukaguzi mkubwa kwenye mipaka. Afrika Kusini ni jirani yetu na tayari kuna kesi nyingi za maambukizi. Alafu kuna eneo la Victoria, na uwanja wake wa ndege ambao unawapokea watalii wengi kutoka nchi za kigeni ambao wanaweza kuwa na virusi hivyo. Kwa hivyo nadhani kabisa kuna umuhimu mipaka ifungwe, " ameongeza daktari huyo.

Kufikia sasa, serikali imepiga marufuku mikusanyiko ya watu zaidi ya 100, lakini haijatangaza kufungwa kwa shule.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.