Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-CORONA-AFYA

Coronavirus: Waziri wa Ulinzi wa Zimbabwe azigeukia nchi za Magharibi

Nchini Zimbabwe, kauli ya Waziri wa Ulinzi kuhusu ugonjwa wa Covid-19 imezua utata. Oppah Muchinguri ameliita janga la Corona kama "adhabu" ya Mungu iliyoletwa hapa duniani kuiadhibu Marekani na Umoja wa Ulaya, kwa kuiwekea vikwazo nchi yake.

Waziri wa Ulinzi wa Zimbabwe Oppah Muchinguri Desemba 15, 2019 huko Harare.
Waziri wa Ulinzi wa Zimbabwe Oppah Muchinguri Desemba 15, 2019 huko Harare. herald.co.zw
Matangazo ya kibiashara

"Ugonjwa wa Corona ni kazi ya Mungu, ambaye ameadhibu nchi ambazo zimetuwekea vikwazo," amesema Waziri Oppah Muchinguri. Waziri wa Ulinzi alikuwa akizungumza katika mkutano wa mwishoni mwa wiki Kaskazini mwa Zimbabwe.

Marekani imeendelea kuweka vikwazo dhidi ya watu karibu 100 wa Zimbabwe na vyombo vya kisheria kwa karibu miaka ishirini, ikiwa ni pamoja na rais wa sasa Emmerson Mnangagwa. Mwanzoni mwa mwezi huu, Washington iliongeza vikwazo hivyo kwa mwaka mmoja, hasa kwa sababu ya kukandamiza upinzani.

"Wamekuwa wafungwa wa nyumbani. Uchumi wao umedhoofika kama walivyoathiri uchumi wetu. Wanapaswa kuhisi athari za ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Covid-19 ili kuelewa maumivu tunayo." kauli ambayo imeendelea kukosolewa kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa siku kadhaa, raia wa Zimbabwe wamekuwa wakilalamika juu ya ya serikali yao kushindwa kutekeleza majukumu yake. Hakuna kesi hata moja ya Covid-19 ambayo imeripotiwa nchini Zimbabwe, lakini nchi jirani ya Afrika Kusini, inaendelea kuathirika na ugonjwa huo, ambapo mwishoni mwa wiki iliyopita kesi zaidi ya hamsini zilithibitishwa.

Siku ya Jumatatu alaasiri, rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa alijaribu kurekebisha kauli ya waziri wake, bila kumtaja akisema kwamba hakuna mtu anayeweza kulaumiwa kutokana na janga hili, ambalo halina mipaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.