Pata taarifa kuu
CHINA-AFYA

Mlipiko wa virusi vya Corona vyaua mtu wa nne China

Mzee mwenye umri wa miaka 89 amekuwa mtu wa nne kupoteza maisha nchini China kutokana na ugonjwa wa virusi vipya vya Corona ambavyo vimeenea nchini humo na mataifa jirani.

Idadi ya watu ambao wamegunduliwa kuambukizwa na virusi vya Corona imeongezeka hadi watu 218.
Idadi ya watu ambao wamegunduliwa kuambukizwa na virusi vya Corona imeongezeka hadi watu 218. AFP Photo/Noel Celis
Matangazo ya kibiashara

Maofisa wa afya nchini China wanasema mzee huyo alipoteza maisha kwenye mji wa Wuhani ambako ndiko kwa mara ya kwanza virusi hivi viliripotiwa, ambapo mpaka sasa watu zaidi ya 200 wameambukizwa.

Kamati ya dharura ya shirika la Afya Duniani WHO, itakutana wiki hii kujadili mlipuko wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vipya vya aina ya Corona.

Homa hiyo inayofananishwa na ugonjwa wa SARS unaosababisha ugumu wa kupumua, imeenea zaidi China.

Mamlaka nchini humo sasa zimethibitisha wasiwasi uliokuwepo awali kuwa virusi hivi vinavyofanana na vile vya homa ya mafua ya ndege, sasa vinaambukizwa kutoka kwa binadamu mmoja kwenda mwingine, tangazo linalozidisha hofu ya kutokea mlipuko mkubwa zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.