Pata taarifa kuu

Liberia: Bunge la Seneti laidhinisha kuundwa kwa mahakama ya uhalifu wa vita vya wenyewe kwa wenyewe

Maseneta wa Liberia walipiga kura kwa kauli moja siku ya Jumanne Aprili 9 kwa azimio ambalo linalenga kuunda mahakama ya kuhukumu uhalifu uliofanyika wakati wa vita viwili vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo, kuanzia mwaka 1989 hadi mwaka 1996 na kuanzia mwaka 1999 hadi mwaka 2003.

Liberia haijawahi kushughulikia uhalifu uliofanyika wakati wa vita viwili vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo, lakini hukumu zimetolewa nje ya nchi. Hapa mmoja wa wahusika katika vita hivyo akisikilizwa katika kesi huko Tampere, Finland, mnamo Machi 12, 2020.
Liberia haijawahi kushughulikia uhalifu uliofanyika wakati wa vita viwili vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo, lakini hukumu zimetolewa nje ya nchi. Hapa mmoja wa wahusika katika vita hivyo akisikilizwa katika kesi huko Tampere, Finland, mnamo Machi 12, 2020. © Mika Kanerva / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ikiwa wabunge walikuwa tayari wamepiga kura ya kuunga mkono ombi hili la muda mrefu kutoka kwa jumuiya ya kimataifa, kura ya Seneti ilikuwa ya mshangao kwa sababu viongozi wengi wa zamani wa waasi au wa kivita sasa ni maseneta.

Jumuiya ya kimataifa na waathiriwa kwa muda mrefu wametoa wito wa kuundwa kwa mahakama hiyo, maombi ambayo hadi sasa yamepuuzwa. Lakini miaka 20 baada ya matukio hayo, Rais Joseph Boakaï alitangaza wakati wa kuapishwa kwake mwezi Januari kuundwa kwa ofisi yenye jukumu la "kuchunguza uwezekano" wa mahakama hii. Mwezi uliopita, Bunge pia lilipiga kura kuunga mkono sheria ya utekelezaji wake.

Kura hii katika Bunge la Seneti ni zaidi ya hatua muhimu: ni jambo la kushangaza kidogo kwa sababu viongozi wa zamani wa waasi au wa kivita ambao walikuwa washiriki wa migogoro wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Liberia sasa wanashikilia nyadhifa za juu nchini humo.

Mfano na Prince Johnson, aliyehusishwa katika ripoti kadhaa za uchunguzi. Leo ni seneta, alionya mwezi uliopita dhidi ya "hatari za kudhoofisha" kwa hatua kama hiyo. Hata hivyo siku ya Jumanne, alijirudii na kuipigia kura azimio ambalo linalenga kuunda mahakama hii maalum. Ikiwa mradi huo utafanikiwa, anaweza kujikuta kizimbani.

Licha ya vifo 250,000 na maelfu ya waathiriwa bado wako hai, hakuna hukumu iliyotangazwa nchini Liberia. Mahakama za Libeŕia haziwezeshwi bila kupitishwa kwa sheŕia ya kuanzisha mahakama maalum. Walakini,  baadhi ya uhalifu ulishughulikiwa nje ya nchi.

Safari ya kutunga sheria ya uundaji huu bado ni ndefu. Azimio lililopigiwa kura katika Bunge la Seneti lazima sasa lirejee kwa Bunge la taifa ambalo litapisha marekebisho yaliyofanywa na maseneta. Azimio hili la sasa pia litawasilishwa ili kuidhinishwa na Rais Joseph Boakaï kabla ya kuandikwa kwake. Hili likishafikiwa, itabidi lijadiliwe na kupigiwa kura tena na mabunge hayo mawili.

"Ni wakati wa Liberia kupitisha sheria hii na kusonga mbele", 

amesema Alain Wermer, wakili na mkurugenzi wa shirika la Civitas Maxima.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.