Pata taarifa kuu

Liberia: Kuelekea kuundwa kwa mahakama maalum ya kuhukumu uhalifu wa vita vya wenyewe kwa wenyewe?

Nchini Libeŕia, waathiriwa wamekuwa wakidai hili kwa zaidi ya miaka 20: kuundwa kwa mahakama maalum ya kuwahukumu wahusika wa uhalifu wa vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vilisababisha vifo vya zaidi ya watu 250,000. Bunge la Libeŕia lilipitisha hoja juu ya hili, na kuongeza matumaini ya Walibeŕia kuwa hatimaye kuweza kushuhudia haki katika ardhi yao.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vilisababisha vifo vya zaidi ya watu 250,000, Liberia.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vilisababisha vifo vya zaidi ya watu 250,000, Liberia. AFP - ALAIN BOMMENEL
Matangazo ya kibiashara

Hadi sasa, mahakama za kigeni zina jukumu la kuwashtaki wababe wa zamani wa vita. Paris kwa sasa inamhukumu kamanda wa zamani wa waasi Kunti Kamara katika ngazi ya rufaa. Sasa jukumu hilo linaweza kuangukia Liberia yenyewe, kutokana na hoja iliyopitishwa siku ya Jumanne, ambayo inaleta matumaini na mashaka.

Mwanaharakati wa haki za binadamu Maxson Kpakio amekuwa akisubiri kuundwa kwa mamlaka hiyo tangu mwaka 2009. Mwaka huo, Tume ya Ukweli na Maridhiano ilichapisha ripoti iliyopendekeza kufunguliwa mashtaka kwa wahalifu dhidi ya ubinadamu. Pendekezo halikufanyiwa kazi. Kwa hoja iliyopitishwa na Bunge la Liberia, matumaini ya haki yanazaliwa upya kwa Maxson Kpakio, ambaye alimpoteza mjomba wake wakati wa vita vya kwanza vya wenyewe kwa wenyewe, katika eneo la Lofa, mojawapo ya mikoa kulikoripotiwa mauaji mengi.

“Moja wapo ya makundi yanayopigana yalijaribu kumsajili mjomba wangu, lakini alikataa. Alisema dini yake haikumruhusu kuua, anasema Maxson Kpakio. Walimfunga, wakamfunika macho na kumtesa. Walimtia katika maji yanayochemka na ndivyo alivyouawa, kwa sababu tu alikataa kushiriki katika vita. "

Alikuwa na umri wa miaka 16 mjombake alipoteswa na kuuawa na kundi la waasi la Ulimo. Anasema yuko tayari kufanya lolote ili kupata haki: “Bado ninahisi uchungu wa kifo cha mjomba wangu leo. Mpaka nipate haki, mpaka nisimame mahakamani na kumuuliza mhusika "kwanini umefanya hivyo?", sijui amani. Na watu wengi waliuawa katika wilaya yangu ya Foya, katika mkoa wa Lofa. Nafsi yangu haitapumzika kwa amani hadi watu walipe gharama ya uhalifu wao. "

Mfumo wa kisheria uliyofafanuliwa

Liberia haijawahi kumhukumu yeyote kati ya wauaji. Wababe wengi wa zamani wa vita wanachukua nyadhifa muhimu, na hivyo kuchochea hisia za kutokujali. Ikiwa Bunge litapiga hatua kuelekea haki, Oscar Bloh, mwanasheria, ana mashaka: “Sheria lazima iwe wazi: mamlaka ya mahakama hii itakuwa yapi? Je, itaundwa na majaji wa Liberia au majaji wa kimataifa? Vipi kuhusu ulinzi wa mashahidi? Liberia inakaribia kufanya kazi kubwa na lazima tuhakikishe kwamba mfumo wa kisheria unatii. "

Hoja hiyo sasa itajadiliwa na Bunge la Seneti kabla ya kuwasilishwa kwa Rais Joseph Boakai. Rais huyu aliahidi kupigana dhidi ya kutokujali wakati wa kampeni yake ya uchaguzi. Matarajio ambayo yanatiliwa shaka na wachambuzi, kwa sababu ya ukaribu wake na mbabe wa vita mwenye nguvu na seneta, Prince Johnson.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.