Pata taarifa kuu

Ivory Coast: Omba omba wapigwa marafuku mjini Abidjan

Nairobi – Mamlaka katika mji mkuu wa Ivory Coast, Abidjan, imepiga marafuku omba omba kwenye mji huo katika kile inachosema ni hatua ya kujaribu kurejesha mpangilio wa mji.

Abidjan ni mojawapo wa miji yenye idadi kubwa ya raia barani Afrika, ikiwa na wakaazi milioni sita.
Abidjan ni mojawapo wa miji yenye idadi kubwa ya raia barani Afrika, ikiwa na wakaazi milioni sita. AFP - ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Naibu gavana wa mji huo, Vincent N'cho Kouaoh, amesema aina yoyote ya omba omba imepigwa marafuku kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa raia pamoja na kurahisisha shughuli za trafiki na usafiri.

Mwaka wa 2013, wizara ya usalama wa ndani nchini humo, ilipiga marafuku omba omba katika makutano ya barabara lakini ilishindwa kutekeleza agizo hilo.

Mataifa mengine barani Afrika yamechukua hatua kama hii lakini utekelezwaji wake umeonekana kukawama.

Hatua hii imekuja baada ya mamlaka pia kwenye mji huo kubomoa vibanda ambavyo vilikuwa vimejengwa bila idhini.

Abidjan ni mojawapo wa miji yenye idadi kubwa ya raia barani Afrika, ikiwa na wakaazi milioni sita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.