Pata taarifa kuu

Gambia: Sheria dhidi ya ukeketaji yasitishwa

Wabunge wa Gambia walitathmini katika Bunge la taifa Jumatatu Machi 18, 2024 kuondolewa kwa marufuku ya ukektaji nchini. Hatua hii hatimaye haikupigiwa kura na, kwa mujibu wa taarifa zetu, itaenda kwa kamati kwa ajili ya kupiga kura, ambayo tarehe yake haijatangazwa. Mamia ya watu walikusanyika mjini Banjul kupinga marekebisho ya sheria hiyo. Kwa nini wabunge wa Gambia wanarejea kwenye marufuku hii ya ukeketaji ya mwaka wa 2015?

Jumatatu hii, Wabunge wa Gambia walitathmini siku ya Jumatatu katika Bunge la taifa kuondolewa kwa marufuku ya ukeketaji nchini Chad.
Jumatatu hii, Wabunge wa Gambia walitathmini siku ya Jumatatu katika Bunge la taifa kuondolewa kwa marufuku ya ukeketaji nchini Chad. unicef.fr
Matangazo ya kibiashara

Mbunge aliyewasilisha mswada huu anatumia hoja za kidini na kimila. Kulingana na mbune huyo na mashirika ya kidini, kupiga marufuku tabia hii kunakiuka haki ya watu wa Gambia kutekeleza utamaduni wao na mila iliyokita mizizi.

Kwa hakika, ukeketaji umeendelea kutekelezwa kwa wingi nchini Gambia, hata tangu kupigwa kwake marufuku: 73% ya wasichana na wanawake wa Gambia wenye umri wa miaka 15 hadi 49 wamekeketwa nchini humo. Wengi wao walikuwa kabla ya umri wa miaka 5 kulingana na takwimu za 2024 kutoka shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto.

Mashirika mengi ya kiraia yanazitaka mamlaka kutokubali shinikizo kutoka kwa makundi yenye msimamo mkali. 

Anna Njie, Mkuu wa chama cha Wanasheria Wanawake nchini Gambia, ambaye alishiriki kikao cha bunge siku ya Jumatatu, alitangaza kwamba yeye na wenzake walikuwa wameongoza "vita vikali vya kukuza haki za wanawake na wasichana ili Gambia iwe moja ya nchi zinazoheshimu mikataba ya kimataifa. Na tunaedelea kujitolea kuhakikisha kuwa sheria hii haifanyiwi marekebisho.”

Sheria ya 2015 inayoharamisha ukeketaji wa viungo vya uzazi inasema kwamba mhusika yeyote wa ukeketaji aadhibiwe kwa kifungo cha hadi miaka mitatu au alipe faini ya dalasi 50,000, sarafu ya Gambia. Kifungo cha maisha kinaweza kutolewa ikiwa msichana anafariki dunia baada ya kitendo hicho.

"Miaka ya utetezi yasalia bila majibu"

Mashirika yote ya wanawake yaliyohojiwa katika bara la Afrika, iwe nchini Mali, Togo, Gambia na Senegal, yanasema yameghadhabishwa.

Mtandao wa mashiŕika ya wanawake ya Afŕika Maghaŕibi, ambayo wanachama wake kwa sasa wanakutana katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York kutathmini matarajio ya kuongeza kasi ya uwezeshaji wa wanawake, wana wasiwasi mkubwa. Mtandao wa Wildaf, mtandao wa kutetea haki za wanawake barani Afrika, umejibu katika taarifa kwa vyombo vya habari kwa kutoa msaada kwa wanawake wa Gambia.

Kwa mujibu wa Oumou Touré, mratibu wa shirika la FemiLead Mali, hii ni "miaka ya utetezi isiyokuwa na majibu". Hofu ya mashirika ya kutetea haki za wanawake ni kwamba hatua hii ya kuharamisha ukeketaji itaenea katika bara zima la Afrika. Kwa sababu tabia hii ya ukeketaji, ingawa imepigwa marufuku katika nchi nyingi, bado inafanywa kwa na watu wengi.

Kulingana na UNICEF, zaidi ya wanawake milioni 230 wamekeketwa duniani kote. milioni 144 barani Afrika. Kwa mujibu wa shirika la Plan International, kuongeza ufahamu wa matokeo mabaya, kimwili na kisaikolojia, pamoja na kuimarisha mfumo wa sheria (hata kama adhabu ni chache), kungewezesha kupunguza idadi ya watu wanaokeketwa duniani. Kila mwaka, zaidi ya wasichana au vijana milioni 3 hukeketwa kote ulimwenguni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.