Pata taarifa kuu

Chad: UN kusitisha msaada wa chakula kwa wakimbizi wa Sudan kutokana na ukosefu wa fedha

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limetangaza siku ya Jumanne kwamba litalazimika kusitisa mwezi Aprili msaada wake kwa mamia ya maelfu ya wakimbizi waliowasili nchini Chad kutoka Sudan wakitoroka vita na kutoa wito wa michango ili kuepuka " janga kabisa "kutokana na matatizo ya kifedha".

Baadhi ya misaada inayotolewa na Mpango wa Chakula Duniani inaweza kuonekana katika kambi ya Adré nchini Chad.
Baadhi ya misaada inayotolewa na Mpango wa Chakula Duniani inaweza kuonekana katika kambi ya Adré nchini Chad. © REUTERS
Matangazo ya kibiashara

"Mchanganyiko wa mgogoro wa Sudan unalemea mwitikio wa kibinadamu nchini Chad, ambao tayari unafadhiliwa vibaya na umelemewa," limesema shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na msaada wa chakula kwa watu waliokimbia makazi yao kutokana na migogoro au umaskini baada ya maafa.

"Kutokana na matatizo ya kifedha, msaada wa WFP kwa wakimbizi milioni 1.2 wa Sudan na watu walioathiriwa na mgogoro huo, ikiwa ni pamoja na wakimbizi wapya kutoka Sudan, utasitishwa mwezi Aprili," WFP imesema katika taarifa yake.

"Tunahitaji wafadhili ili kuzuia hali kuwa janga kubwa," limeongeza,likikadiria "hitaji la dharura la dola milioni 242" na kutaja "mbio dhidi ya wakati."

Kulingana na WFP, maelfu ya wakimbizi wa Sudan wanaendelea kuvuka mpaka na kuingia Darfur, na kadiri msimu wa mvua unavyokaribia, hii itafanya njia za kupeleka misaada ya kibinadamu katika kambi za mashariki mwa Chad na Darfur kusiwe na njia ya kupitika.

Chad, ambayo inahifadhi idadi kubwa zaidi ya wakimbizi wa Sudan, tayari imehifadhi zaidi ya 400,000 kabla ya mzozo mpya.

Kulingana na hesabu yake, "baada ya kuzuka kwa mzozo mkali nchini Sudan (Aprili 15, 2023), zaidi ya wakimbizi 559,000 wa Sudan na 150,000 waliorejea Chad waliingia Chad". Ni "mojawapo ya idadi kubwa ya wakimbizi inayokua kwa kasi zaidi barani Afrika", inasisitiza WFP.

Wimbi la wakimbizi linaongeza matatizo ya Chad katika kulisha wakazi wake. Nchi iliyo nusu jangwa katika Afrika ya Kati, wakaazi wanakabiliwa na "mwaka wa tano mfululizo wa shida ya chakula", inasisitiza WFP.

Katikati ya mwezi wa Februari, rais wa mpito wa Chad Mahamat Idriss Déby Itno alitangaza "hali ya dharura ya chakula na lishe" nchini kote.

Nchi hiyo ni makazi ya wakimbizi wa ndani na wakimbizi wengi wa ndani kutokana na migogoro inayoendelea nchini humo na miongoni mwa majirani zake, Sudan, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Niger, Nigeria, Libya na Cameroon.

"Kwa miezi kadhaa, wakimbizi wengi kutoka Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Nigeria hawajapokea msaada wowote kutokana na ukosefu wa fedha," inabainisha WFP. Na "kupunguza mgao kunachochea ushindani kati ya wakimbizi, wanaorejea na jajii zinazowapokea juu ya rasilimali ambazo tayari ni chache, hivyo basi kuchochea mvutano na ukosefu wa utulivu."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.