Pata taarifa kuu

Waasi wa M23 wadhibiti eneo jingine la Kibirizi mashariki mwa DRC

Waasi wa M23 wamedhibiti eneo jingine la Kibirizi, wakati mapigano yakiendelea kwa siku ya tatu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Hayo yanajiri wakati maelfu ya raia wanaendelea kutoroka makaazi yao kufuati mapigano hayo wakikimbilia maeneo salama.

Watu wameyatoroka makazi yao huko Kibirizi, katika mkoa wa Kivu Kaskazini.
Watu wameyatoroka makazi yao huko Kibirizi, katika mkoa wa Kivu Kaskazini. Laval P/Rudipresse
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na tovuti ya Deutsche Welle kwa Kiswahili kufikia jana Alhamis, M23 walikuwa wameudhibiti mji wa Kibirizi, ulioko kilometa karibu 30 upande wa Kaskazini Mashariki. 

Kulingana na shirika la habari la AFP likinukuu afisa mmoja wa utawala katika eneo hilo, M23 walidhibiti mji huo baada ya kufyatuliana risasi na wanajeshi wa Kongo na wapiganaji wanaoiungamkono serikali. Mkazi mwingine Gervais Kambale  eneo la karibu la Kanyabayonga ambalo raia wanaokimbia wamekuwa wakiwasili kwa wiki nzima akinukuliwa na AFP kutoka, amesema wameshuhudia mamia ya watu waliokuwa njiani kuelekea upande wa kaskazini. 

Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya watu 100,000 wamekosa makaazi wiki hii, wengi ni kutoka mji wa Nyanzale katika mkoa wa Kivu Kaskazini, Mashariki mwa DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.