Pata taarifa kuu
MAPIGANO-USALAMA

Waasi wa M23 wauteka mji wa Nyanzale, mashariki mwa DRC

Baada ya mapigano ya siku mbili, mji wa Nyanzale, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, umeangukia mikononi mwa waasi wa M23, na kusababisha "zaidi ya watu 100,000 kukimbia", shirika la Umoja wa Matafa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA limesema siku ya Jumatano.

Kichanga, Kivu Kaskazini, DR Congo: Mwanajeshi wa FARDC aatoa ulinzi kwa  raia karibu na Nyanzale.
Kichanga, Kivu Kaskazini, DR Congo: Mwanajeshi wa FARDC aatoa ulinzi kwa raia karibu na Nyanzale. Photo MONUSCO/Abel Kavanagh
Matangazo ya kibiashara

"Zaidi ya watu 100,000" wametoroka makazi yao mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo katika kipindi cha siku mbili kufuatia kuzuka kwa mapigano, shirika la Umoja wa Matafa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA.

Kamanda wa jeshi la DRC, Jerome Chico Tshitambwe alithibitisha kwa shirika la habari la Reuters kwamba Nyanzale imetekwa na waasi.

Nyanzale, ambayo iko kilomita 130 (maili 80) kaskazini mwa mji wa Goma, ilikuwa ni kimbilio la watu waliotoroka makazi yao kutokana na mapigano katika maeneo jirani.

Wapiganaji wa M23 walichukua silaha tena mwaka wa 2021, wakilalamikia kuvunjwa kwa ahadi katika mkataba wa amani wa awali.

Wapiganaji wa M23 wana vifaa vya kutosha, lakini kundi hilo linakanusha kuwa kuwa na ushirikiano na Rwanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.