Pata taarifa kuu

Sudan: UNSC yatoa wito wa kusitishwa kwa mapigano 'haraka' kabla ya Ramadhani

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa wito siku ya Ijumaa, Machi 8, kwa usitishaji "mara moja" wa mapigano nchini Sudan wakati wa mwezi wa Ramadhani, ambao unaanza mapema wiki ijayo.

Des partisans de la résistance populaire armée soudanaise, qui soutient l'armée, circulent sur des camions à Gedaref, dans l'est du Soudan, le 3 mars 2024, dans le cadre du conflit qui oppose actuelle
Wafuasi wa kundi la Sudanese Armed Popular Resistance, linalounga mkono jeshi, wakipanda malori huko Gedaref, mashariki mwa Sudan, Machi 3, 2024, huku kukiwa na mzozo unaoendelea kati ya jeshi na vikosi vya wanamgambo vya RSF. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Azimio hilo limepitishwa kwa kura 14 za ndio na moja ya ambayo imejieuia kuonyesha msimamo wake, Urusi. Nakala hiyo "inataka kusitishwa mara moja kwa uhasama kabla ya mwezi wa Ramadhani" na inaomba "wahusika wote kwenye mzozo kutafuta suluhu la kudumu la mzozo huo kupitia mazungumzo".

Siku ya Alhamisi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alitoa wito kwa wapiganaji nchini Sudan kwa ajili ya kusitisha mapigano wakati wa mwezi wa Ramadhani, kuheshimu "maadili" ya mwezi mtukufu kwa Waislamu wakati mzozo wa kibinadamu unafikia viwango vya mgogoro mkubwa. 

Sudan ilitumbukia kwenye machafuko mwezi Aprili mwaka jana, wakati mvutano wa muda mrefu kati ya jeshi lake linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah Burhan na vikosi vya wanamgambo, (RSF) vinavyoongozwa na Mohammed Hamdan Dagalo vilipoingia katika mapigano ya mitaani katika mji mkuu, Khartoum.

Mapigano hayo yameenea katika maeneo mengine ya nchi, hususan maeneo ya mijini, lakini katika eneo la Darfur, magharibi mwa Sudan, yamechukua sura tofauti, kwa mashambulizi ya kikatili ya vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), ambao wengi wao ni Waarabu, dhidi ya raia wenye asili ya Afrika. Maelfu ya watu waliuawa.

Miaka 20 iliyopita, Darfur ilifanana na mauaji ya halaiki na uhalifu wa kivita, hasa uliofanywa na wanamgambo wa Kiarabu wa Janjaweed dhidi ya watu wanaojitambulisha kama Afrika ya Kati au Mashariki.

Mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu Karim Khan alisema mwishoni mwa mwezi wa Januari kwamba kuna sababu ya kuamini kwamba pande zote mbili katika mzozo wa sasa zinafanya uhalifu wa kivita unaowezekana, uhalifu dhidi ya ubinadamu au mauaji ya halaiki huko Darfur.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.