Pata taarifa kuu

Vita nchini Sudan: Abdel Fattah al-Burhan arejea katika mji mkuu

Nchini Sudan, mkuu wa majeshi almezuru mji mkuu wa nchi hiyo Februari 8, baada ya kufanya ziara kadhaa nje ya nchi kutafuta uungwaji mkono katika vita kati ya wanajeshi wake dhidi ya wanamgambo wa Mohamed Hamdan Dogolo Hemedti tangu Aprili 15, 2023.

Mkuu wa jeshi la Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan akizungumza mjini Khartoum, Sudan, Desemba 5, 2022.
Mkuu wa jeshi la Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan akizungumza mjini Khartoum, Sudan, Desemba 5, 2022. AP - Marwan Ali
Matangazo ya kibiashara

 

Nchini Sudan, kamanda mkuu wa jeshi, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, amezuru mji mkuu wa Sudani,  Khartoum mnamo Februari 8, 2024. Amekagua gwaride la jeshi huko Omdurman, na maeneo mengine kaskazini mwa mji mkuu Khartoum, kulingana na taarifa ya jeshi.

Akitumia fursa hiyo, kwa mara nyingine tena amekanusha jaribio lolote la mapinduzi au kukamatwa, mapema mwezi wa Februari, maafisa wa jeshi lake wamesema.

Jenerali al-Burhan alihamia huko Port Sudan, kaskazini-magharibi mwa nchi, tangu mwezi Agosti mwaka jana, kama vile baraza kuu na serikali.

Ziara yake mjini Khartoum inalenga zaidi ya yote kupunguza mvutano ndani ya jeshi, huku akisisitiza juu ya ukweli kwamba lina umoja katika kukabiliana na Vikosi vya Msaada wa Haraka ambavyo vimekuwa vikikabiliana navyo tangu Aprili 15, 2023.

Ni marejeo ambayo yanaweka taji la maendeleo ya hivi karibuni ya jeshi la Sudan huko Khartoum na hasa huko Omdurman, dhidi ya wanamgambo wanaoongozwa na Hemedti, vinasema vyanzo vya karibu na jeshi.

Hata hivyo vyombo vya habari vya ndani vinabaini kwamba madhumuni "yasiyo rasmi" ya ziara hii yanalenga "kufuta athari zote za mapinduzi ya kijeshi" au angalau kupunguza athari ya kukamatwa kwa maafisa kadhaa wakuu waliohusika na mpinduzi hayo.

Jenerali al-Burhan pia alijaribu kuongeza ari ya askari wake. Aliahidi kuwatibu waliojeruhiwa katika vikosi vya jeshi na "kung'oa wanamgambo wa waasi" na "mamluki wao", akimaanisha FSR na washirika wao.

Pia ametembelea ngome na kambi za kijeshi huko Wadi Saydna, Omdurman, ambapo kambi muhimu ya jeshi iko na ambapo kunazinduliwa operesheni zake katika mji mkuu dhidi ya RSF.

Jenerali al-Burhan anajiandaa kuzuru Tehran hivi karibuni, ikiwa ni sehemu ya ziara mpya ambayo pia itampeleka Uturuki pamoja na nchi zingine za ukanda huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.