Pata taarifa kuu
USALAMA-HAKI

DRC: Wanawake wawili wanaoshutumiwa uchawi wachomwa moto katika kijiji cha Kivu Kusini

Wanawake wawili wenye umri wa miaka 60 na 65, wanaotuhumiwa uchawi, wamepigwa mawe na kisha kuchomwa moto hadharani siku ya Jumapili katika kijiji cha Kivu Kusini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kulingana na vyanzo kadhaa vilivyohojiwa siku ya Jumatatu.

Wanawake hawa wawili waliuawa kwa sababu walishutumiwa na sehemu ya watu kwa kufanya uchawi na "kuhusika na vifo vya watu kadhaa" katika jamii.
Wanawake hawa wawili waliuawa kwa sababu walishutumiwa na sehemu ya watu kwa kufanya uchawi na "kuhusika na vifo vya watu kadhaa" katika jamii. LIONEL HEALING / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa usiku, kundi la vijana kutoka Nyamutiri "waliwapiga mawe wanawake hawa na kuchoma miili yao baada ya kuwatoa nje ya nyumba zao", kulingana na shirika la habari la AFP, likimnuku André Byadunia, kiongozi wa shirika la kiraia huko Uvira, makao makuu ya eneo ambapo matukio yalifanyika. .

Alibainisha kuwa wanawake hawa wawili waliuawa kwa sababu walituhumiwa na sehemu ya watu kufanya uchawi na "kuhusika na vifo vya watu kadhaa" katika jamii.

"Jivu linaondolewa kwenye eneo la mkasa," amesema Makelele Murande, katibu tawala wa kichifu cha Bafuliru, ambapo wanawake hao wawili waliuawa, amehojiwa kwa njia ya simu Jumatatu mchana. "Polisi na jeshi hawakuweza kuingilia kati kwa wakati ili kuwaokoa wanawake hawa wawili," amelaumu naibu mkuu wa eneo la Uvira, Timothée Bakanirwa.

Maandamano yalizuka baadaye, yaliyoandaliwa na "watu waliowaua" wanawake hao wawili, ameeleza Kelvin Bwija, kiongozi wa mashirika ya kiraia katika eneo hilo. Kulingana mwanaharakati huyo, waandamanaji walilalamika kwamba "wachawi wanaodaiwa kukamatwa kila mara huachiliwa na idara za usalama."

Makelele Murande amebaini kwamba "kutokana na jeshi kuingilia kati", vizuizi vya waandamanaji vimeondolewa na kwamba "hali imerejea kuwa shwari". Kulingana na Nelly Adidja, wa Chama cha Wanawake katika vyombo vya Habari (AFEM) cha Kivu Kusini, wanawake 33 walioshutumiwa uchawi waliuawa katika mkoa huo mwaka wa 2023, na "wengine wengi walifukuzwa kutoka vijijini mwao na kuishi katika kutanga-tanga".

Rais wa mashirika ya kiraia huko Uvira anakemea "kitendo hiki ambacho kimepitwa na wakati", huku akitaka tabia hiyo isitishwe. Bw. Byadunia anatoa wito kwa "wahalifu wa kitendo hiki" kufunguliwa mashitaka na anasikitika "kuwazika wanawake waliouawa", huku "mwezi mahsusi kwa wanawake" ukianza.

Mnamo mwaka wa 2021, Profesa Bosco Muchukiwa, mwanasosholojia na mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Juu ya Maendeleo ya Vijijini (ISDR) ya Bukavu, anaona "kuibuka tena kwa jambo hilo" ambalo amehusisha na kushindwa kwa Serikali katika "misheni zake kuu", kwa sababu, "polisi na vyombo vya sheria hawafanyi kazi yao ipasavyo".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.