Pata taarifa kuu

RDC : Wanawake kutoka maeneo yanayokabiliwa mapigano waliwasilisha malalamiko kwa rais

Nairobi – Wanawake nchini DRC, hasa kutoka maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo ambako kunashuhudiwa utovu wa usalama, mwishoni mwa juma lililopita, waliwasilisha malalamiko yao kwa rais Felix Tshisekedi, wakitaka wasaidiwe kukomesha vitendo vya ubakaji na ukatili mwingine wanaofanyiwa na makundi yenye silaha.

Wanawake hao wanataka wasaidiwe kukomesha vitendo vya ubakaji na ukatili mwingine wanaofanyiwa na makundi yenye silaha
Wanawake hao wanataka wasaidiwe kukomesha vitendo vya ubakaji na ukatili mwingine wanaofanyiwa na makundi yenye silaha © Alexis Huguet, AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika visa vingi, walionusurika walisema walishambuliwa na watu wenye silaha walio wadhalilisha kingono,kama anavyoeleza mama huyu mkimbizi  anaye ishi sasa ndani ya kambi moja nje kidogo na mji wa Goma .

"Kila mwanamke anayo haki yakuishi,tunahitaji kurudi nyumbani kwetu masisi.” alisema mmoja wa akina mama wakimbizi.

00:18

Mmoja wa akina mama wakimbizi

Nyumba na ukosefu wa bidhaa muhimu, vimekuwa pia ni changamoto kwa wanawake hao wanaokabiliwa na changamoto za vita.

“Wanawake tunalala uwanjani, ndani ya nyumba za hema ambamo mawe yamejaa kwa wingi, ni mateso mno." alieleza mama mwengine mkimbizi.

00:10

Mama mwengine mkimbizi nchini DRC

Pasy Mubalama ni kutoka shirika la wanawake Tujitetee huko kivu kaskazini.

"Sisi kama vile wanawake tumechoshwa na vita ni vizuri sasa suluhu ipatikane." alieleza Pasy Mubalama.

00:10

Pasy Mubalama ni kutoka shirika la wanawake Tujitetee

Tangu mwaka wa 2023 kufikia sasa, shirika hilo pamoja na idara ya maswala ya kijamii jimboni,zimekadiria kuwa zaidi ya visa 25000 vya ukatili wa kijinsia vimeripotiwa  kutokana na vita vinavyosambaa  katika baadhi ya maeneo  mkoani kivu kaskazini.

 Benjamin Kasembe-RFI Kiswahili, Goma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.