Pata taarifa kuu

Chad: Mahamat Idriss Déby, atangaza kugombea uchaguzi wa urais mnamo Mei 6

Mkuu wa utawala wa kijeshi madarakani tangu mwaka 2021, Jenerali Mahamat Idriss Déby Itno, rais wa mpito, ametangaza katika hotuba yake kwamba atakuwa mgombea katika uchaguzi wa urais mnamo Mei 6.

Rais wa Baraza la Mpito la Chad, Mahamat Idriss Deby Itno, akihudhuria sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 63 ya Uhuru  wa Chad huko Ndjamena, Agosti 11, 2023.
Rais wa Baraza la Mpito la Chad, Mahamat Idriss Deby Itno, akihudhuria sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 63 ya Uhuru wa Chad huko Ndjamena, Agosti 11, 2023. © Denis Sassou Gueipeur / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Mimi, Mahamat Idriss Déby Itno, nitakuwa miongoni mwa wagombea uchaguzi wa urais wa 2024 chini ya bendera ya muungano wa vyama vya For a United Chad," amesema baada ya vyama 221 vinavyounda muungano huu kumtaka agombee kwenye kiti cha urais.

Wakati huo akiwa na umri wa miaka 37, alitangazwa kuwa rais wa mpito na utawala wa kijeshi anaoongoza wa majenerali kumi na watano mnamo Aprili 20, 2021, baada ya kutangazwa kwa kifo cha baba yake, Marshal Idriss Déby Itno, kiongozi wa taifa, rais wa Chad kwa miaka thelathini, amvaye aliuawa na waasi akiwa njiani kuelekea kwenye uwanja wa vita.

Mahamat Déby mara moja aliahidi kurudisha mamlaka kwa raia kupitia uchaguzi baada ya kipindi cha mpito cha miezi kumi na minane, lakini muda huu ulipotamatika, aliuongeza kwa miaka miwili. Takriban miaka mitatu baadaye, utawala wake wa kijeshi umemuondoa au kumtenga kisiasa mpinzani yeyote, na upinzani unamtuhumu kwa kuendeleza "utawala wa Déby". Anaonekana kuazimia kufuata nyayo za baba yake na kujiandaa kwa utawala mrefu.

Uhalali unaoyumba

Lakini uhalali wake ndani ya familia ya Déby na kabila lake, Zaghawa, ambao wametawala nchi hiyo kwa mkono wa chuma kwa miaka thelathini na tatu, umekuwa ukiyumba tangu jeshi kumuua binamu yake na adui Yaya Dillo siku ya Jumatano, katika shambulio dhidi ya makao makuu ya chama chake cha upinzani.

Ili kudhihirisha mamlaka yake, aliwaondoa majenerali kadhaa watiifu kwa baba yake katika jeshi lenye nguvu zote ambalo uongozi wake unaaminiwa na Wazaghawa na baadhi ya washirika wa kabila la Goran. Wakati fulani aliwabadilisha na kuwaweka majenerali kutoka kabila la Goran, hatua ambayo kiasi fulani iliwahuzunisha Wazaghawa. Mahamat ni nusu Zaghawa upande wa baba yake na nusu Gorane upande wa mama yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.