Pata taarifa kuu

Mpinzani mkuu wa serikali ya Chad auawa katika shambulio la jeshi dhidi ya chama chake

Mpinzani wa serikali ya kijeshi Yaya Dillo Djérou amefariki nchini Chad katika shambulio dhidi ya makao makuu ya chama chake, miezi miwili kabla ya uchaguzi wa urais, ambaye alikuwa anaonekana kama mpinzani mkuu wa rais wa mpito, Jenerali Mahamat Idriss Déby Itno, binamu yake mwenyewe.

Yaya Dillo Djerou ni binamu wa Jenerali Mahamat Idriss Déby Itno.
Yaya Dillo Djerou ni binamu wa Jenerali Mahamat Idriss Déby Itno. © AFP - Thomas Coex
Matangazo ya kibiashara

Utulivu umerejea siku ya Alhamisi siku moja baada ya kifo chake, baada ya siku ya mvutano mkali katikati ya mji mkuu N'Djamena ambapo idadi kubwa ya jeshi lilivuka katikati ya jiji na kuzingira makao makuu ya Chama cha Kisoshalisti Bila Mipaka (PSF) cha Bw. Dillo.

Ilikuwa ni majira ya alasiri, baada ya kukata mtandao katika jiji lote kutokana na watu kupiga simu kutaka kuingilia kati kuja "kumlinda" mpinzani, askari walishambulia makao makuu kwa bunduki za kivita katikati ya makabiliano na wafuasi wa chama hicho, huku risasi za hapa na pale zilisikika kulingana na waandishi wa shirika la habari la AFP.

Yaya Dillo alifariki ajificha

Yaya Dillo alifariki dunia "ambapo alikuwa amekimbilia, katika makao makuu ya chama chake. Hakutaka kujisalimisha na kuwafyatulia risasi polisi," Waziri wa Mawasiliano Abderaman Koulamallah ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Alhamisi. 

Polisi walikuwa wamekuja kumkamata mwanaharakati wa PSF ambaye serikali ilikuwa imemtuhumu kwa "jaribio la kumuua" Rais wa Mahakama ya Juu siku kumi zilizopita. Baadaye serikali ilimshutumu Yaya Dillo kwa kutekeleza shambulizi usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi dhidi ya makao makuu ya idara ya ujasusi, ANSE, kulipiza kisasi kwa kukamatwa kwake. Shambulio hili, lililofanywa na Bw. Dillo kwa mujibu wa serikali, lilisababisha "vifo kadhaa", kulingana na serikali ambayo haikubainisha katika kambi gani.

Saa chache kabla ya kifo chake, Bw. Dillo alikanusha vikali shutuma hizi kwa shirika la habari la AFP na kushutumu "uongo" na "mchezo wa kuigiza" kilichokusudiwa kumtenga kugombea kwake katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Mei 6. Tarehe hiyo ilitangazwa siku ya Jumanne. Bw. Dillo, 49, mara kwa mara alishutumu uchaguzi utakaogubikwa na udanganyifu kwa kumpa ushindi Bw. Déby. Alidai kufanyiwa marekebisho kwa kalenda hii huku akithibitisha kuwa atakuwa mgombea dhidi ya jenerali huyo kijana.

Mahamat Déby, wakati huo alikuwa na umri wa miaka 37, alitangazwa kuwa mkuu wa nchi na jeshi mnamo Aprili 20, 2021 baada ya kutangazwa kwa kifo cha baba yake, Marshal Idriss Déby Itno, aliyeuawa wakati akienda vitani dhidi ya waasi. Idriss Déby Itno alitawala nchi hii kubwa ya Saheli kwa mkono wa chuma kwa zaidi ya miaka 30.

Akiwa bado hajatangazwa kuwa rais katika uongozi wa utawala wa kijeshi unaoongozwa na majenerali 15, Mahamat Déby aliahidi kurejesha mamlaka kwa raia kupitia uchaguzi baada ya kipindi cha mpito cha miezi 18. Lakini miezi 18 baadaye, alirefusha kwa miaka miwili, na hakuficha tena nia yake ya kugombea urais. Upinzani ulishutumu "muendelezo wa utawala wa ukoo" wa Déby.

"Mchezo wa kuigiza"

Katika ujumbe wa sauti uliotumwa kwa shirika la habari la AFP saa chache kabla ya kifo chake, Bw. Dillo alidai kwamba "watawala" na rais wa Mahakama ya Juu walifanya "mchezo wa kuigiza" "kwa kudai kuwa kulifanyika uvamizi dhidi ya ofisi ya hakimu mkuu, wakati ambapo hata hakujeruhiwa, ili kuhalalisha kubatilisha ugombea wake wa urais.

Shambulio hilo dhidi ya makao makuu ya PSF lilikuja miaka mitatu baada ya shambulio kama hilo lililofanywa na wanajeshi katika makao makuu ya Bw. Dillo na chama chake, ambapo mama yake na mwanawe mmoja waliuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.