Pata taarifa kuu

Waasi wa Tuareg wanashutumu jeshi na Wagner kwa kuwaua watu 7 kutoka Chad na Niger

Waasi wa Tuareg kaskazini mwa Mali walishutumu jeshi na kundi la wanamgambo wa Urusi Wagner siku ya Jumatano kwa kuwaua raia saba wa Chad na Niger katika mashambulizi ya ndege zisizo na rubani kwenye mpaka wa Algeria.

Mapigano yalianza tena Agosti 2023 baada ya miaka minane ya utulivu kati ya Bamako na makundi ya waasi yaliyona idadi kubwa ya Watuareg, ambao walishindania udhibiti wa eneo na kambi za kijeshi zilizoachwa na walinda amani wa Umoja wa Mataifa.
Mapigano yalianza tena Agosti 2023 baada ya miaka minane ya utulivu kati ya Bamako na makundi ya waasi yaliyona idadi kubwa ya Watuareg, ambao walishindania udhibiti wa eneo na kambi za kijeshi zilizoachwa na walinda amani wa Umoja wa Mataifa. © AFP PHOTO / Souleymane AG ANARA
Matangazo ya kibiashara

 

Likipigiwa simu siku ya Jumatano na shirika la habari la AFP kuhusu madai haya yaliyotolewa na Mfumo wa Kimkakati wa Kudumu (CSP), muungano wa makundi yenye waasi yenye silaha ya Tuareg, jeshi la Mali halikujibu.

Wakati wa usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano, "muungano wa kigaidi wa Wagner-FAMA (majeshi ya Mali) yalifanya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani kwenye kituo cha mauzo ya mafuta huko Talhandak", kijiji cha njia panda kilichoko kwenye eneo kubwa la jangwa kaskazini mwa Mali, muungano wa makundi ya waasi umebaini katika taarifa kwa vyombo vya habari.

"Kosa hili la kumi na moja kwa watu wasio na hatia lilisababisha vifo vya watu saba wa mataifa ya Chad na Niger pamoja na wahasiriwa wengine ambao bado wako chini ya vifusi," kinaongeza chanzo hicho. CSP inalaani "vitendo hivi vya kigaidi vinavyorudiwa na serikali ya Bamako ambavyo vinalenga tu watu wasio na hatia na miundombinu ya kiraia."

Mapigano yalianza tena mwezi Agosti 2023 baada ya miaka minane ya utulivu kati ya Bamako na waasi wengi wa Tuareg, ambao walishindania udhibiti wa eneo na kambi za kijeshi zilizoachwa na walinzi wa amani wa Misheni ya Umoja wa Mataifa waliotakiwa kuondoka na utawala wa kijeshi uliyoko madarakani nchini Mali. Wanajeshi waliochukua madaraka kwa nguvu mwaka 2020 walipata mafanikio ya kiishara yaliyosifiwa sana nchini Mali, lakini waasi hawakuweka silaha zao chini na kutawanyika katika eneo la jangwa na milima la kaskazini.

Vikosi vya Mali viliungwa mkono na mamluki wa Wagner kulingana na waasi na maafisa waliochaguliwa wa eneo hilo, ingawa uwatala wa kijeshi unakanusha uwepo katika nchi hii ya kundi la usalama la kibinafsi la Urusi na vitendo vyake viovu vinavyokosolewa. Mashambulizi kaskazini mwa Mali yalikumbwa na tuhuma nyingi za dhuluma dhidi ya raia zinazofanywa na vikosi vya Mali na washirika wao wa Urusi, shutuma zilizokanushwa na serikali ya Bamako.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.