Pata taarifa kuu

DRC: Ombi la kuachiliwa kwa muda kwa mwanahabari Stanis Bujakera lakataliwa

Mwandishi wa habari wa Kongo Stanis Bujakera bado yuko kizuizini mjini Kinshasa baada ya ombi lake la kuachiliwa kwa muda kukataliwa siku ya Jumanne, mawakili wake wamesema.

Moja ya mitaa ya eneo la Gombe, eneo la biashara ya Kinshasa, ambako kunapatikana jela anakozuiliwa Stanis Bujakera.
Moja ya mitaa ya eneo la Gombe, eneo la biashara ya Kinshasa, ambako kunapatikana jela anakozuiliwa Stanis Bujakera. REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Mwandishi wa Gazeti la Jeune Afrique, anakabiliwa na mashitaka kwa makala ambayo hayajatiwa saini kwa jina lake, akihusisha ujasusi wa kijeshi katika mauaji ya mwanasiasa wa upinzani Chérubin Okende. "Tunatumai kwamba agizo la kuachiliwa kwa muda kwa mteja wetu (...) litatolewa leo," Wakili Jean-Marie Kabengela, mmoja wa mawakili wa mwandishi wa habari, aliviambia vyombo vya habari siku ya Jumatatu jioni.

Lakini "kwa sababu za kiufundi kutoka mahakama, kwa namna moja au nyingine, uamuzi huu utatolewa siku ya kesho" (Jumanne), aliongeza, baada ya kukaa mchana mzima katika mahakama kuu ya Kinshasa-Gombe. “Tumetulia,” alisema Bw. Kabengela.

Mawakili wake waliwasilisha ombi jipya la kuachiliwa siku ya Ijumaa, wakati wa kusikilizwa kwa kesi yake, siku moja baada ya tamko la Rais Félix Tshisekedi ambaye alisema mwandishi huyo wa habari amesalia jela kutokana na "kutowajibika kwa vyombo vya sheria" nchini DRC.

Rais aliongeza kuwa "atafuatilia mwenyewe kesi hiyo", na kutoa matumaini ya kuachiliwa kwake hivi karibuni. Kimsingi, mahakama ilikuwa na saa 48 kutoa uamuzi. Tangu kukamatwa kwake Septemba 8, wito umeongezeka wa kuachiliwa kwa Stanis Bujakera, lakini maombi yake yote ya kuachiliwa kwa muda hadi sasa yamekataliwa.

Stanis Bujakera pia mwandishi wa shirika la habari la kimataifa la REUTERS na naibu mkurugenzi wa vyombo vya habari vya mtandaoni vya Kongo Actualité.cd, anatuhumiwa "kutengeneza na kusambaza" taarifa ya kijasusi ya kiraia inayohusisha ujasusi wa kijeshi katika mauaji ya Chérubin Okende, aliyepatikana amefariki mnamo Julai 13 kwenye gari lake akiwa na majeraha ya risasi. Utetezi wa mwandishi wa habari umekuwa ukipinga shutuma hizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.