Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Kinshasa: Kesi ya mwanahabari Bujakera yahirishwa tena hadi Januari 12, 2024

Katika kesi ya mwanahabari Stanis Bujakera wa Gazeti la lugha ya kifaransa la Afrique na Actualité.cd, mahakama kuu ya Kinshasa-Gombe imeamua tena Ijumaa hii Desemba 22 kuahirisha kesi hiyo hadi Januari 12 kwa ajili ya uchambuzi wa ripoti ya mtaalam aliyepewa kazi ya uthibitishaji wa nyaraka, muhuri na sahihi ya huduma za idara ya Ujasusi (ANR).

Mwandishi wa habari wa DRC Stanis Bujakera.
Mwandishi wa habari wa DRC Stanis Bujakera. © Avec l'aimable autorisation de actualite.cd
Matangazo ya kibiashara

Mwanahabari huyo sasa anazuiliwa katika gereza kuu la Makala kwa zaidi ya siku 100, bila kufunguliwa mashtaka.

Siku ya Ijumaa wakili wa mshtakiwa ameomba kesi hiyo ichunguzwe kulingana na uhalali wake, badala ya kubaki kwenye fomu kila wakati.

Stanis Bujakera anashtakiwa kwa kueneza "uvumi wa uongo" na kusambaza habari za uongo zinazohusisha shirika la ujasusi wa kijeshi kuhusu mauaji ya aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi Chérubin Okende. Hii ni makala, ambayo haijatiwa saini na mwandishi wa habari, kulingana na taarifa yake, iliyochapishwa katika Gazeti la Jeune Afrique juu ya suala hilii, inayonukuu ripoti juu ya mkasa huu, unaohusishwa na idara ya upelelezi (ANR). Hati hii itatiliwa shaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.