Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

DRC: Mwanahabari Stanis Bujakera azuiliwa kinyume cha sheria, kulingana na utetezi wake

Wiki nne baada ya kukamatwa kwake, upande wa utetezi wa mwandishi wa habari wa DRC Stanis Bujakera, mwandishi wa Gazeti la Jeune Afrique mjini Kinshasa, unabaini kwamba kuzuiliwa kwa mteja wake ni kinyume cha sheria na kuomba tena aweze kuchiliwa kwake.

Mwandishi wa habari wa DRC Stanis Bujakera Tshiamala.
Mwandishi wa habari wa DRC Stanis Bujakera Tshiamala. © Avec l'aimable autorisation de actualite.cd
Matangazo ya kibiashara

"Mteja wetu anazuiliwa kinyume cha sheria," Bw. Ndikulu Yana alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari siku ya Ijumaa jioni.

Mnamo Septemba 15, mahakama iliamuru mwandishi wa habari kuzuiliwa siku 15, wakili huyo amekumbusha, akisikitishwa na kuwekwa gerezani zaidi ya muda huu bila uhalali wowote wa kisheria, amesema.

Stanis Bujakera, pia naibu mkurugenzi wa kitengo cha uchapishaji cha tovuti ya habari ya Kongo Actualité.cd na mwandishi wa shirika la habari la REUTERS mjini Kinshasa, anashutumiwa hasa kwa "kughushi" na "kueneza uvumi wa uongo", kwa makala yaliyochapishwa na Gazeti la Jeune Africa kwa kuweka mashakani ujasusi wa kijeshi katikati ya mwezi wa Julai kuhusiana na mauaji ya mwanasiasa wa upinzani Chérubin Okende.

Makala hayo yalitokana na hati iliyowasilishwa kama hati ya siri kutoka kwa idara nyingine ya kijasusi. Mamlaka inadai kuwa hati hii ni bandia.

Me Yana pia aliona kwamba mashtaka dhidi ya Stanis Bujakera yalikuwa kinyume na kanuni zote za kisheria, kwa kuwa makala husika haikutiwa saini na mwandishi wa habari. "Haiwezekani kumshtaki mtu kwa mambo ambayo yalifanywa na wengine," wakili huyo amesema.

Upande wa mashtaka, pia amelalamika, ulisema ulitambua simu ya mwandishi huyo kuwa ndiyo ya kwanza kusambaza hati hiyo ya siri. Lakini, kwa njia "isiyoeleweka na hata inayokinzana", ofisi ya mashitaka inasema pia kwamba Stanis Bujakera alipokea hati hii kutoka kwa akaunti ya Telegraph.

Alipokamatwa Septemba 8, Stanis Bujakera alihamishwa wiki moja baadaye kwenda katika jela la Makala, gereza kubwa zaidi mjini Kinshasa, ambako amekuwa akizuiliwa tangu wakati huo. Mahakama mara mbili zilikataa ombi la kuachiliwa kwa muda kwa mwanahabari huyo, kwa misingi kwamba anaweza kutoroka.

Mawakili wa Stanis Bujakera wanapinga hukumu hiyo na kwa mara nyingine tena waliomba mahakama siku ya Ijumaa"kumuachilia kwa muda ili kumruhusu kuripoti mahakamani katika kesi inayosalia kama mtu huru".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.