Pata taarifa kuu

Hali ya wasiwasi yatanda kufuatia kimbunga Eleanor kupiga Mauritius

Safari za ndege zmefutwa na shule kufungwa: Mauritius inajiandaa siku ya Alhamisi kwa ajili ya kuwasili kwa kimbunga cha kitropiki Eleanor, ambacho kilitarajiwa kukumba nchi hii ndogo katika Bahari ya Hindi saa sita mchana kulingana na huduma za hali ya hewa.

Mnamo mwezi wa Januari, Kimbunga Belal kiliua mtu mmoja katika kisiwa hiki, maelfu ya watu walijikuta hawana umeme na magari mengi yalizama kwenye maji.
Mnamo mwezi wa Januari, Kimbunga Belal kiliua mtu mmoja katika kisiwa hiki, maelfu ya watu walijikuta hawana umeme na magari mengi yalizama kwenye maji. © AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Uwanja wa ndege wa kimataifa wa kisiwa hicho umefungwa tangu 7:30 asubuhi saa za ndani, mamlaka ya uwanja wa ndege, Airport of Mauritius Ltd (AML) imetangaza. Shirika la ndege la kitaifa la Air Mauritius limefuta safari mbili za ndege zilizokuwa zimepangwa asubuhi.

Kulingana na taarifa ya hivi punde iliyotolewa na huduma za hali ya hewa, kimbunga kikali cha kitropiki lilikuwa saa 4:00 Alfajiri kwa saa za huko kilomita 200 kaskazini mashariki mwa kisiwa hicho, ikielekea kusini-magharibi kwa kasi ya kilomita 20 kwa saa. Kilitarajiwa kupita sehemu yake ya karibu na kisiwa wakati wa mchana.

"Upepo utavuma kutoka kusini-mashariki mwanzoni kwa kasi ya karibu kilomita 40 kwa saa na kufikia kilomita 110 km kwa saa wakati wa mchana, na kuimarisha kuzidi kilomita 120 kwa saa," inabainisha mamlaka ya hali ya hewa.

Nchini Mauritius, vyuo vyote vya elimu na vyuo vikuu vitasalia kufungwa siku ya Alhamisi, na huduma za umma na za kibinafsi kwa likizo ya kulazimishwa, wakati usafiri wa umma hautatolewa.

Mauritius, kisiwa cha kitalii chenye wakazi wapatao milioni 1.3, maarufu kwa fukwe zake za mchanga mweupe na maji safi, kinakabiliwa na vimbunga. Mnamo mwezi wa Januari, Kimbunga Belal kiliua mtu mmoja katika kisiwa hiki, maelfu ya watu walijikuta hawana umeme na magari mengi yalizama kwenye maji.

Na mwaka mmoja uliopita, kisiwa hicho kilikumbwa na mvua kubwa na upepo mkali kutoka kwa Kimbunga Freddy, ambacho kiliharibu Kusini-mashariki mwa Afrika, ikiwa ni pamoja na Malawi, Msumbiji na Madagascar. Takriban dhoruba au vimbunga kumi huvuka Bahari ya Hindi kusini-magharibi kila mwaka wakati wa msimu wa kimbunga, ambao huanzia mwezi wa Novemba hadi mwezi wa Aprili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.