Pata taarifa kuu

Wahamiaji 13 kutoka Sudan wazama pwani ya Tunisia

Nairobi – Wahamiaji 13 kutoka Sudan wamezama maji Pwani ya Tunisia na kupoteza maisha huku wengine 27 hawafahamiki walipo, baada ya boti waliyokuwa wanasafiria kuzama.

Idadi kubwa ya watu wamekuwa wakiripotiwa kuvuka kwenda barani Ulaya kwa kutumia njia hatari
Idadi kubwa ya watu wamekuwa wakiripotiwa kuvuka kwenda barani Ulaya kwa kutumia njia hatari AP - Cecilia Fabiano
Matangazo ya kibiashara

Tukio hili limetokea jana, katika eneo la mji wa pwani wa Monastir.

Maafisa wanasema wahamiaji 42 walikuwa kwenye boti hiyo, na walikuwa wametokea kwenye mji wa Jebiniana, wakielekea barani Ulaya.

Serikali ya Tunisia imebaini kuwa, wahamiaji wote walikuwa raia wa Sudan waliokuwa wamesajiliwa kama waomba hifadhi na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi, na walikuwa wanasafirishwa kinyume cha sheria barani Ulaya, wakati boti yao ilipozama.

Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa, boti waliyokuwa wameabiri ilikuwa imeutengezwa na mabati na vyuma kuukuu, na uchunguzi unaendelea kuwatafuta wale ambao hawajapatikana.

Tunisia na Libya, ndio mlango mkuu unaotumiwa na wakimbizi kwenda Ulaya ambapo maelfu hutatarisha maisha yao kila mwaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.