Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Afrika Kusini: Uandikishaji wa wapiga kura umemalizika bila kujali

Nchini Afrika Kusini, zaidi ya wapiga kura milioni 27.4 wamejiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura. Mwishoni mwa wiki iliyopita, Tume Huru ya Uchaguzi iliandaa kampeni ya mwisho ya usajili wa wapiga kura, kabla ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika miezi ijayo.Tarehe ya upigaji kura bado haijatangazwa, lakini uchaguzi unapaswa kufanyika kabla ya tarehe 8 Agosti.

Mtu huyu akipita mbele ya mabango ya kutaka kuandikishwa kwa wapiga kura kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2024 nchini Afrika Kusini katika kitongoji cha Verulam, karibu na Durban, Februari 3, 2024.
Mtu huyu akipita mbele ya mabango ya kutaka kuandikishwa kwa wapiga kura kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2024 nchini Afrika Kusini katika kitongoji cha Verulam, karibu na Durban, Februari 3, 2024. AFP - RAJESH JANTILAL
Matangazo ya kibiashara

 

Kulingana na Tume Huru ya Uchaguzi ya Afrika Kusini, wapiga kura wapya 457,000 walijiandikisha mwishoni mwa juma lililopita. Miongoni mwao, 77% wana umri wa chini ya miaka 29, wanawake ni wengi kidogo, na idadi kubwa zaidi ya waliojiandikisha wako katika jimbo la KwaZulu-Natal.

"Kampeni ilikuwa ya mafanikio," imekaribisha Tume ya Uchaguzi, ambayo imekumbusha kuwa bado inawezekana kujiandikisha mtandaoni hadi tarehe ya uchaguzi itakapotangazwa.

Hata hivyo, baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaeleza kuwa zaidi ya wapiga kura milioni 27 waliojiandikisha wanawakilisha asilimia 64 pekee ya wapiga kura wanaostahiki. Zaidi ya theluthi moja ya wale ambao wangeweza kupiga kura hawajasajiliwa. Wanaangazia kutojali kwa uchaguzi.

Kwa miaka 30, viongozi wa kisiasa wamekuwa wakitoa ahadi ambazo hawajazitekeleza: kuiondoa nchi katika umaskini; kuendeleza huduma za umma. Lakini leo hii, Waafrika Kusini milioni 18 wanaishi katika hali ya umaskini uliokithiri.

Kura za maoni zinaonyesha kuwa kwa mara ya kwanza chama tawala cha ANC kinaweza kupoteza wingi wake. Tarehe ya uchaguzi inapaswa kutangazwa na mkuu wa nchi wakati wa hotuba yake kuhusu hali ya nchi iliyopangwa siku ya Alhamisi, Februari 8.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.