Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Afrika Kusini: Siku mbili za kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura

Vyama vya siasa nchini Afrika Kusini vimekuwa vikijaribu kuhamasisha wafuasi wao siku ya Jumamosi, siku ya mwisho ya usajili wa wapiga kura kabla ya uchaguzi mkuu ujao.

Jumamosi na Jumapili ni siku za mwisho za usajili wa wapigakura, lakini usajili wa mtandaoni utaendelea hadi tarehe ya uchaguzi itakapotangazwa.
Jumamosi na Jumapili ni siku za mwisho za usajili wa wapigakura, lakini usajili wa mtandaoni utaendelea hadi tarehe ya uchaguzi itakapotangazwa. © EMMANUEL CROSET / AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Miaka 30 baada ya demokrasia kuchukua nafasi ya utawala wa ubaguzi wa rangi nchini humo, uchaguzi wa mwaka huu utaonekana kwa wengi kuwa kura ya maoni ya matokeo ya chama tawala cha African National Congress (ANC).

Kura za maoni zinaonyesha kuwa chama hicho kinaweza kupoteza wengi wao mwaka huu, huku kumbukumbu za vita dhidi ya ubaguzi wa rangi, ambapo kilichukua nafasi kubwa, zikififia na wapiga kura kuzingatia kashfa za hivi majuzi na matokeo duni.

Kiongozi wa chama cha ANC Cyril Ramaphosa amekutana na wafuasi wake siku ya Jumamosi huko Soweto, viungani mwa jiji hilo.

"Mchakato unaendelea vizuri sana," ameliambia shirika la habari la AFP mbele ya umati uliokusanyika mbele ya kituo cha biashara cha Jabulani. Alipoulizwa kuhusu tarehe ya uchaguzi ujao, ambayo bado haijatangazwa, amejibu kwa tabasamu pana: "Hivi karibuni."

Baadhi ya maafisa wa ANC walioshiriki mkutano huo wamebaini kwamba tangazo hilo linaweza kuja siku ya Alhamisi, wakati wa hotuba ya kila mwaka ya hali ya taifa ya Ramaphosa Bungeni mjini Cape Town.

Jumamosi na Jumapili ni siku za mwisho za usajili wa wapigakura, lakini usajili wa mtandaoni utaendelea hadi tarehe ya uchaguzi itakapotangazwa. Huko Fordsburg, kitongoji cha tabaka la wafanyakazi kusini mwa Johannesburg, kituo cha kupigia kura kimeshuhudia watu sita pekee wakijitokeza kujiandikisha au kubadilisha anwani zao katika saa tatu za kwanza za ufunguzi.

Nje ya vituo, ANC na chama kikuu cha upinzani, Democratic Alliance (DA), walijenga vibanga ili kuwahifadhi wanachama wa chama hicho wanaojaribu kuwahimiza wafuasi wao kujiandikisha.

Katika ofisi zote zilizotembelewa na shirika lahabari la AFP, kulikuwa na waangalizi wengi kutoka vyama tofauti kuliko wapiga kura, lakini maafisa kutoka Tume ya Uchaguzi ya Afrika Kusini (IEC) wamesema wako makini. Wengi wao wamependekeza kuwa wazee walikuwa tayari wamesajiliwa na kwamba vijana bado wanaweza kujiandikisha mtandaoni.

"Wanaweza kujiandikisha mtandaoni, lakini kituo hiki kiko wazi kwa watu ambao hawana vifaa," ameelezea Mosa Khunou, afisa wa IEC, baada ya kumsaidia mzee kubadilisha anwani yake kwenye orodha ya uchaguzi.

Uchaguzi mkuu utafanyika ndani ya siku 90 baada ya kumalizika kwa muhula wa Bw Ramaphosa mwezi wa Mei, na katika uchaguzi huo watachagua bunge la kitaifa ambalo nalo litaamua iwapo litaongeza muda wa Bw Ramaphosa au kuidhinisha uteuzi wa rais mpya.

Chama cha ANC kinatarajiwa kusalia kuwa chama kikubwa zaidi lakini, wataalam wanasema, huenda kwa mara ya kwanza kikahitaji kuunda muungano ili kupata wingi wa kura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.