Pata taarifa kuu
RUSHWA-SIASA

Ripoti: Ufisadi nchini Afrika Kusini katika kiwango chake kibaya zaidi katika miaka 12

Ufisadi umefikia kiwango chake kibaya zaidi katika miaka kumi na mbili nchini Afrika Kusini, ambapo uchaguzi mkuu umepangwa katika miezi ijayo, kuungana na nchi ambazo rushwa "imekita mizizi" na huenda "kuenea", kulingana na ripoti iliyochapishwa Jumanne na shirika lisilo la kiserikali la Transparency International

Tume ya uchunguzi kuhusu ufisadi uliokithiri katika kipindi cha miaka tisa madarakani cha aliyekuwa rais Jacob Zuma (2009-2018) ilitoa hitimisho la kutisha mwaka 2022.
Tume ya uchunguzi kuhusu ufisadi uliokithiri katika kipindi cha miaka tisa madarakani cha aliyekuwa rais Jacob Zuma (2009-2018) ilitoa hitimisho la kutisha mwaka 2022. © AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Shirika lisilo la kiserikali linalopambana na ufisadi huchapisha Kielezo cha Mtazamo wa Ufisadi katika nchi 180 kila mwaka, kutathmini kiwango chake katika sekta ya umma kama inavyofikiriwa na wataalamu na ulimwengu wa biashara.

"Afrika Kusini haijawahi kupata alama za chini kiasi hiki" tangu shirika la ndani la Transparency International, Corruption Watch, lilipoanza kazi yake miaka 12 iliyopita katika nchi ambayo sasa imeainishwa kama "demokrasia yenye mapungufu", shirika hili linasisitiza. "Afŕika Kusini sasa inaungana na nchi duniani kote ambako rushwa inaonekana siyo tu kuwa imekita mizizi, lakini yenye uwezo wa kuenea,” Transparency International inaongeza katika ŕipoti yake.

"Inasikitisha kwamba katika nchi ambayo wafisadi wamefichuliwa kupitia michakato ya umma kama vile tume ya Zondo na kupitia uchunguzi wa vyombo vya habari, watu wachache wamefikishwa mahakamani," Karam Singh wa kitengo cha Ufisadi amesema.

Jaji Raymond Zondo aliongoza tume ya uchunguzi kuhusu ufisadi uliokithiri katika kipindi cha miaka tisa ya uongozi wa Rais wa zamani Jacob Zuma (2009-2018) kwa miaka minne. Mnamo mwaka 2022, alitoa hitimisho la kusikitisha lililotolewa kutoka kwa zaidi ya siku 400 za kesi ambapo zaidi ya mashahidi 300 walijitokeza. Rais Cyril Ramaphosa, aliyeitwa kutoa ushahidi mbele ya tume hiyo, aliahidi mara kwa mara kukabiliana na ufisadi. Lakini hakuna mtu aliyekamatwa katika hatua hii.

Kesi za ufisadi pia ni moja ya vipengele vinavyoelezea kupotea kwa nafasi katika uchaguzi wa chama cha kihistoria kilicho madarakani tangu kumalizika kwa utawala wa kibaguzi, ANC. Kikiwa kimetawaliwa na kashfa na hali mbaya ya kijamii na kiuchumi, chama cha African National Congress kiko hatarini kwa mujibu wa kura za maoni kupoteza wingi wake wa wabunge, kwa mara ya kwanza katika historia yake, wakati wa uchaguzi ujao utakaofanyika kati ya mwezi Mei na Agosti.

Raia wa Afrika Kusini watapiga kura kuwachaguwa wabunge wao wapyakatika ngazi ya taifa na mikoa, huku uchaguzi huu ukifungua njia ya kuchaguliwa kwa rais ajaye, atakayeteuliwa na wabunge wa kitaifa na sio kwa upigaji kura wa moja kwa moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.