Pata taarifa kuu

Mkuu wa MONUSCO asisitiza juu ya ulinzi wa raia kabla ya walinda amani kuondoka DRC

Kuondoka kwa walinda amani mashariki mwa DRC lazima kufanyike "sanjari na kuongezeka kwa nguvu" kwa vikosi vya usalama vya DRC, ili ulinzi wa raia uendelee kuzingatiwa, Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Jean Pierre Lacroix amesisitiza Jumamosi huko Bukavu (Kivu Kusini).

MONUSCO bado ina wanajeshi 13,500 na maafisa wa polisi 2,000 nchini DRC.
MONUSCO bado ina wanajeshi 13,500 na maafisa wa polisi 2,000 nchini DRC. © Alexis HUGUET / AFP
Matangazo ya kibiashara

 

"Bado kuna maeneo yasiyokalika" katika mkoa wa Kivu Kusini, ambapo Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO) utaondoka mwishoni mwa mwezi wa Aprili, Jean-Pierre Lacroix amewaambia waandishi wa habari, baada ya mkutano na gavana wa mkoa huo.

"Hii ndiyo sababu ni muhimu sana (...) kwamba kuondoka kwa taratibu kwa askari wa MONUSCO kufanyike sambamba na kuongezeka kwa mamlaka, kwa kasi ile ile, ya vikosi vya jeshi vya Kongo na vikosi vya usalama," ameongeza. "Lengo," amesisitiza, "ni kwamba ulinzi wa raia (...) uendelee kuzingatiwa."

Mpango wa uondoaji wa haraka wa MONUSCO, iliopo DRC kwa takriban miaka 25 na bado imewekwa katika mikoa matatu yenye matatizo mashariki mwa nchi (Ituri, Kivu Kaskazini na Kivu Kusini), ilipitishwa mwishoni mwa mwaka jana, kwa ombi la Kinshasa ambayo inaiona haina nguvu dhidi ya makundi yenye silaha. Awamu ya kwanza ya kuondoka kwa walinda amani inahusu mkoa wa Kivu Kusini, ambapo kami 14 za MONUSCO zitakabidhiwa mamlaka ya Kongo ndani ya miezi mitatu.

"Katika mpango wa kuondoka kwa vikosi ivi vya Umoja wa Mataifa, imepangwa kuwa chombo kinachowakilisha kambi hizi kitahamishiwa kwa mamlaka ya Kongo" na kwamba matumizi ya mitambo hii yatakuwa "ya manufaa kwa wakazi," amesema Jean-Pierre Lacroix.

Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na operesheni za amani alianza ziara ya wiki moja nchini DRC kwa kuzuru Beni, katika mkoa wa Kivu Kaskazini, siku ya Ijumaa. Atakuwa katika mji mkuu Kinshasa wiki ijayo, ambapo anatazamiwa kukutana na Rais Félix Tshisekedi.

MONUSCO bado ina wanajeshi 13,500 na maafisa wa polisi 2,000 nchini DRC. Siku ya Ijumaa, moja ya helikopta zake iliyo kuwa katika misheni ya uokoaji wa kimatibabu iliponea kudondoshwa baada ya kushambuliwa na watau wanaoshukiwa kuwa waasi wa M23 ("Movement ya Machi 23") katika eneo la Masisi, Kivu Kaskazini. Walinda amani wawili wa Afrika Kusini walijeruhiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.