Pata taarifa kuu

Senegal: Watu saba wapoteza maisha baada ya jengo kuporomoka Dakar

Watu saba wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya jengo moja kuporomoka huko Dakar, nchini Senegal, Rais wa nchi hiyo Macky Sall amesema siku ya Jumatano katika ujumbe kwenye ukurasa wake wa X.

Dakar, inakabiliwa na ukuaji wa haraka wa idadi ya watu na uchumi, imepata mlipuko wa ujenzi katika miaka ya hivi karibuni, wakati mwingine kwa njia isiyo sahihi na bila idhini rasmi.
Dakar, inakabiliwa na ukuaji wa haraka wa idadi ya watu na uchumi, imepata mlipuko wa ujenzi katika miaka ya hivi karibuni, wakati mwingine kwa njia isiyo sahihi na bila idhini rasmi. © AFP
Matangazo ya kibiashara

 

"Nimehuzunishwa sana na ajali mbaya ya kuporomoka kwa jengo huko Xaar Yalla, na kusababisha vifo vya watu 7 na majeraha mabaya. Natuma rambirambi zangu za dhati kwa familia za waathiriwa na ninawatakia ahueni ya haraka majeruhi," ameandika Rais Sall.

Jengo hilo liliporomoka usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne saa saba usiku, kamanda wa kikosi cha Zimamoto na Uokoaji huko Dakar, Martial Ndione, ameliambia shirika la habari la AFP. Jengo hilo, ambalo lilikuwa mahali pa kuishi, "lilikuwa likifanyiwa ukarabati. Sehemu ya jengo ilianguka," amesema. Ameliambia shirika la habari la AFP idadi ya muda ya watu 5 waliofariki na kumi na wawili waliojeruhiwa.

Dakar, inakabiliwa na ukuaji wa haraka wa idadi ya watu na uchumi, imepata mlipuko wa ujenzi katika miaka ya hivi karibuni, wakati mwingine kwa njia isiyo sahihi na bila idhini rasmi. Kuporomoka kwa majengo ni jambo la kawaida barani Afrika. Mnamo mwezi Julai 2023, majengo mawili yaliyokuwa yakijengwa yaliporomoka nchini Guinea na kuua watu watano. Watu sita waliuawa katika jengo lililoporomoka nchini Côte d'Ivoire mnamo mwezi wa Julai 2023.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.