Pata taarifa kuu
SENEGAL-MAFURIKO-MAJANGA ASILI

Mafuriko nchini Senegal: Mkutano wa dharura waitishwa katika ikulu ya rais

Nchini Senegal, viongozi wametolewa wito juu ya usimamizi wa mafuriko. Mvua kubwa zilizonyesha mwishoni mwa wiki iliyopita zilisababisha uharibifu mkubwa na karibu kila sehemu ya nchi imeathirika.

Nyumba nyingi huko Dakar ziko chini ya maji, huku mvua zikiendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini Senegal, Septemba 6, 2020.
Nyumba nyingi huko Dakar ziko chini ya maji, huku mvua zikiendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini Senegal, Septemba 6, 2020. REUTERS/ Zohra Bensemra
Matangazo ya kibiashara

Kutokana na hali hiyo rais Macky Sall amekutana na mawaziri mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani, na Waziri wa Maji na Usafi wa Mazingira, kujadili kuhusu mafuriko ya mwishoni mwa wiki iliyopita, na kutathmini mpango wa miaka kumi wa kudhibiti mafuriko.

Mpango huu, uliozinduliwa na Rais Macky Sall mwenyewe wakati wa kuwekwa kwake kwa kipindi cha miaka kumi (2012-2022), unajumuisha kiasi cha Faranga za CFA Bilioni 767, kulingana na katibu mkuu katika ikulu ya rais, sawa na zaidi ya Euro Bilioni moja.S

Swali linaloulizwa na watu walioathirika na mafuriko hayo, na viongozi wengine wa upinzani, je! pesa hizi zilitumika kwa kazi gani? Waziri Mkuu wa zamani Abdoul Mbaye aamebaini kwamba fedha hizo "hazikutumika kamwe," na "mafuriko yalisitishwa kuwa kipaumbele" baada ya kuondoka kwake serikalini.

Muungano wa Jotna / Wazalendo wa Mbadala wa Ousmane Sonko unatoa wito wa kuundwa kwa utaratibu wa kudhibiti bajeti ambayo itatengwa kwa misaada, ili kuepuka ubadhirifu wowote wa mali ya umma.

Kwa upande wake, serikali inajitetea. Katika mkutano, msemaji wa rais Abdou Latif Coulibaly ameelezea kuwa mvua zilizonyesha mwishoni mwa wiki wiki iliyopita zilikuwa "za kipekee".

Katibu mkuu katika ikulu ya rais amebaini kwamba mafuriko hayo yamesababishwa na "mabadiliko ya hali ya hewa" na amehakikisha kuwa kazi tayari iliyofanywa, kwa mifereji ya maji, kuhifadhi maji na usafi wa mazingira, imewezesha kupunguza uharibifu.

Kwa sasa, serikali inajaribu kushughulikia dharura hiyo. Siku ya Jumatatu Waziri wa Mambo ya Ndani alitangaza njia za ziada za kusukuma maji katika maeneo yenye mafuriko. Kulingana na Aly Ngouille Ndiaye, kufikia sasa vifo sita vinavyohusiana na mvua vimerekodiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.