Pata taarifa kuu

Cameroon: Hervé Bopda, anayeshukiwa kwa 'idadi kubwa sana' ya ubakaji akamatwa

Hervé Bopda, mfanyabiashara wa Cameroon anayeshutumiwa kwa unyanyasaji wa kingono na ubakaji mwingi alikamatwa Jumatano asubuhi huko Douala, imetangaza CRTV, redio na televisheni ya serikali ya Cameroon.

Hervé Bopda alikuwa akifanya kazi katika eneo la Douala. Hapa, mwanamke huyu anatembea katika mitaa ya mji huu magharibi mwa Cameroon, Januari 27, 2022.
Hervé Bopda alikuwa akifanya kazi katika eneo la Douala. Hapa, mwanamke huyu anatembea katika mitaa ya mji huu magharibi mwa Cameroon, Januari 27, 2022. © Charly Triballeau / AFP
Matangazo ya kibiashara

 

"Hervé Bopda alikamatwa asubuhi ya leo (...) huko Bonabéri. Hervé Bopda anashukiwa kuwabaka au kuwalawiti idadi kubwa sana ya wasichana wadogo. Tangu kuanza kwa kesi hiyo (...) waranti mbili za kukamatwa zilitiwa saini. Kukamatwa kwake kunafungua njia kwa taratibu za kisheria ambazo zitahusika kuorodhesha shahidi dhidi yake."

Chama cha Wanasheria wa Cameroon kilitoa wito wiki iliyopita kwa ajili ya kufunguliwa kwa uchunguzi. Tume ya Haki za Kibinadamu nchini Cameroon pia ilichukua kesi hiyo mnamo Januari 19 kufuatia athari zake kwenye mitandao ya kijamii na ikasikitishwa siku ya Jumamosi ya wiki iliyopita kwamba haikuweza "kushuhulikiwa inavyopaswa", ambayo ni "kuwasikiliza mashahidi" na "kukabili pande zote" kwa kutokujulikana kwa shutma.

Serikali pia ilijibu kupitia Waziri wa mwenye dhamana ya Kuendeleza Wanawake na Familia ambaye alikaribisha "kujihusisha kwa mamlaka za mahakama zenye uwezo kwa nia ya kuthibitisha ukweli wa mambo", katika taarifa iliyochapishwa siku ya Ijumaa.

Marie-Thérèse Abena Ondoa "aliwahimiza" waathiriwa "kuvunja ukimya" na "kutoa kwa mamlaka ya mahakama shahidi na vielelezo muhimu ili kufanya taratibu zinazokusudiwa kuthibitisha ukweli wa mambo". Tangu katikati ya mwezi wa Januari, zaidi ya shuhuda 70 zisizojulikana zenye tuhuma za unyanyasaji wa kingono zimesambazwa kwenye mitandao ya kijamii na mwanablogu wa Cameroon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.