Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Cameroon: Shambulio la watu wanaotaka kujitenga lasababisha kifo cha mtu mmoja Buea

Kundi la wapiganaji wanaotaka kujitenga lilifanya uvamizi usiku wa Januari 29 kuamkia Jumanne Januari 30, 2024 huko Buea, mji mkuu wa Kusini-Magharibi mwa Cameroon, moja ya mikoa miwili ya nchi inayozungumza Kiingereza. Waliwashambulia raia, na kuua angalau mtu mmoja na kujeruhi watu kadhaa. Maelezo.

Muonekano wa angani wa Buea nchini Cameroon, mnamo mwaka wa 2019.
Muonekano wa angani wa Buea nchini Cameroon, mnamo mwaka wa 2019. UNOCHA via Getty Images - Giles Clarke
Matangazo ya kibiashara

 

Na mwandishi wetu wa Yaoundé, Polycarpe Essomba

Usiku ulikuwa wenye msukosuko huko Buea, mji mkuu wa Kusini-Magharibi, mojawapo ya mikoa miwili ya Cameroon inayozungumza Kiingereza: kundi dogo la wapiganaji wanaotaka kujitenga walivamia usiku wa Jumatatu Januari 29 kuamkia Jumanne Januari 30, 2024. Waasi hao walishambulia raia kabla ya usiku kuingia, bila kusababisha hasara lakini walifanya uharibifu wa mali.

Kulingana na vyanzo kadhaa, huko Buea, kundi dogo la washambuliaji walivamia mji huo karibu saa nne usiku siku ya JUmattu. Walilenga eneo lililo karibu na soko kubwa linalopatikana karibu na uwanja wa Molyko, ambapo biashara chache zilifunguliwa. Bernard Okalia Bilai, gavana wa mkoa huo, ambaye alithibitisha taarifa hii kwa RFI, anabainisha kuwa washambuliaji walikuwa na "silaha za kivita". Walifyatua risasi bila tahadhari kwa raia, na kuua angalau mtu mmoja na kujeruhi wengine kadhaa kabla ya kutoweka porini, kinaongeza chanzo hicho.

Washambuliaji hao pia walichoma moto magari yaliyokuwa yameegeshwa hapo. Angalau magari matano yameteketea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.