Pata taarifa kuu

Mafuriko nchini Kongo: Watu 350,000 wanahitaji msaada wa kibinadamu

Zaidi ya watu 350,000 wanahitaji msaada wa dharura wa kibinadamu nchini Kongo-Brazzaville ambapo 3/4 ya idara za nchi hiyo "ziko chini ya maji" kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha, Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa (OCHA) limeonya.

Idara tisa kati ya 12 za nchi bado zimesalia "chini ya maji" na "jumla ya watu milioni 1.8 wameathiriwa" na mafuriko.
Idara tisa kati ya 12 za nchi bado zimesalia "chini ya maji" na "jumla ya watu milioni 1.8 wameathiriwa" na mafuriko. © AFP
Matangazo ya kibiashara

 

"Mafuriko yamewaacha watu bila makazi au kutopata huduma za afya ya msingi. Vijiji, shule na vituo vya afya vimejaa maji, na vituo vingi vya maji na vifaa vya vyoo havifanyi kazi tena," imesema OCHA wakati wa mkutano huko Geneva. Kulingana na OCHA, "zaidi ya watu 350,000 wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu, lakini upatikanaji ni mgumu kutokana na mafuriko na vijiji vingi vinafikiwa kwa boti au mtumbwi."

Kiasi cha "dola milioni 3.6 kutoka kwa Hazina Kuu ya Kukabiliana na Dharura zimetengwa kujibu mahitaji ya dharura zaidi ya watu 270,000" walioathirika, OHA imesema huku ikikadiria kuwa "ufadhili zaidi wa kimataifa utahitajika" kwa suluhisho la kudumu. Mvua kubwa inayonyesha tangu mwezi Oktoba imezamisha kingo karibu na Mto Oubangui, kijito cha Mto Kongo. Mvua hizi pia zimesababisha maporomoko ya udongo ambayo yalisomba nyumba kaskazini mwa Brazzaville hasa.

Hali ya hatari ilitangazwa rasmi na serikali ya Kongo mnamo Desemba 29. Mamlaka kisha ikatangaza kwamba serikali itatoa FCFA bilioni 2.4 (euro milioni 3.6) kusaidia waathiriwa. Takriban wiki tatu baadaye, idara tisa kati ya 12 za nchi bado zimesalia "chini ya maji" na "jumla ya watu milioni 1.8 wameathirika," inabainisha OCHA.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa ushirikiano na serikali ya Brazzaville wameandaa mpango wa kukabiliana matukio hayo, yenye "bajeti ya jumla ya takriban dola milioni 26" na kuamua kuwa sekta za kipaumbele ni pamoja na, miongoni mwa zingine, nyumba na usafi wa mazingira, kulingana na OCHA. Mafuriko haya pia yanaweza kuwa na matokeo ya muda mrefu, kulingana na chanzo hiki ambacho kinakadiria kuwa "heka 2,300 za ardhi inayolimwa zimejaa maji", na kuzua hofu ya kushuka kwa uzalishaji wa kilimo katika miezi ijayo.

Mafuriko haya pia yanaathiri Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, nchi ambayo iko ng'ambo ya Mto Kongo. Katika mji mkuu wa Kinshasa, maeneo ya watalii na maeneo ya makazi bado yako chini ya maji, kutokana na mafuriko ya kipekee. Mafuriko makubwa ya mwisho katika eneo hilo yalianza mnamo mwaka 1961.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.