Pata taarifa kuu

Congo: Watu 37 wafariki katika mkanyagano wakati wa kuandikishwa kwa jeshi Brazzaville

Takriban vijana 37 wa Congo waliuawa usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne katika mkanyagano wakati wa operesheni ya kuwasajili wanajeshi katika mji mkuu Brazzaville, mamlaka ya Kongo imetangaza Jumanne, Novemba 21.

Maafisa wa Polisi wa Kongo wakiwakagua vijana huko Brazzaville mnamo Aprili 4, 2016.
Maafisa wa Polisi wa Kongo wakiwakagua vijana huko Brazzaville mnamo Aprili 4, 2016. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Idadi ya muda iliyotangazwa na idara ya huduma za dharura inaonyesha watu 37 wamefariki na wengi kujeruhiwa," inabaini taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kitengo maalumu kinachoongozwa na Waziri Mkuu Anatole Collinet Makosso, akisema ni "janga" kwa nchi ya Congo.

Kuajiri vijana 1500

Picha nyingi, zilizoshirikiwa kwenye mitandao ya kijamii, zinaonyesha makumi ya miili ya watu waliofariki iliyohifadhiwa kwenye chumba cha maiti cha manispa ya mji wa Brazzaville, pamoja na watu waliojeruhiwa waliolazwa katika kituo cha hospitali ya chuo kikuu (CHU) cha Brazzaville na hospitali ya kijeshi. Jeshi la Kongo lilitangaza wiki iliyopita kuajiri vijana 1,500 wenye umri wa miaka 18 hadi 25.

Jumatatu usiku, vijana waliokuwa wakijiandikisha waliiingia kwa nguvu na kuvunja lango la uwanja wa soka Michel d'Ornano, ambapo zozi hilo linafanyika, katikati mwa jiji la Brazzaville. Mkanyagano ulitokea, ambapo watu wengi walianguka na kukanyagwa, wakaazi wamesema. Baadhi ya waliojeruhiwa wako katika hali mbaya, kulingana na shuhuda kutoka familia za waathiriwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.