Pata taarifa kuu

Afrika Kusini imethibitisha visa viwili vya maambukizi ya kipindupindu

Nairobi – Raia nchini Afrika Kusini wametakiwa kuchukua tahadhari baada ya mamlaka kwenye taifa hilo kuthibitisha visa viwili vya ugonjwa wa kipindupindu kaskazini mwa wilaya ya Limpopo.

Mamlaka imeeleza kuwa visa vyote viwili vilitokea nchini Zimbabwe, taifa ambalo linakabiliwa na msambao wa kipindupindu
Mamlaka imeeleza kuwa visa vyote viwili vilitokea nchini Zimbabwe, taifa ambalo linakabiliwa na msambao wa kipindupindu © WHO Zimbabwe
Matangazo ya kibiashara

Idara ya afya katika wilaya hiyo imesema kuwa wagonjwa wote wawili ni raia wa Zimbabwe walioingia kwenye hilo kupitia maeneo ya mpakani.

Aidha idara hiyo ya afya imeeleza kuwa kisa cha kwanza kilithibitishwa baada ya mgonjwa mwenye umri wa miaka 43 kupatikana na maambukizi hayo baada ya kufanyiwa vipimo.

Kisa cha pili kilikuwa cha mwanaume mwengine mwenye umri wa miaka 27 ambao wote kwa sasa wametengwa hosipitalini.

Mamlaka imeeleza kuwa visa vyote viwili vilitokea nchini Zimbabwe, taifa ambalo linakabiliwa na msambao wa kipindupindu.

Kipindupindu kwa sasa kimesababisha vifo vya watu 200 nchini Zimbabwe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.