Pata taarifa kuu

Zambia kupokea dozi za chanjo ya kipindupindu kutoka WHO

Nairobi – Zambia inatarajiwa kupokea dozi milioni moja za chanjo dhidi ya kipindupindu kutoka kwa shirika la afya duniani WHO.

Nchi hiyo inapokea dozi milioni moja za chanjo ya kipindupindu kutoka WHO
Nchi hiyo inapokea dozi milioni moja za chanjo ya kipindupindu kutoka WHO REUTERS - Denis Balibouse
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja wakati huu taifa hilo likikabiliwa na mlipuko wa ugonjwa huo ambao umesababisha vifo vya watu 249 tangu mwezi Oktoba mwaka jana.

Kwa mujibu wa Roma Chilengi, mshauri wa rais Hakainde Hichilema kuhusu masuala ya afya, dozi hizo zitapelekwa katika maeneo ambayo yameripoti visa vingi vya maambukizi.

Aidha mshauri huyo wa rais amethibitisha kuwa dozi hizo zinatarajiwa kuwasili siku ya Jumamosi.

Serikali kwenye taifa hilo imechelewesha kufunguliwa kwa shule na kutangaza mikakati mipya ya kuzuia maambukizo ya kipindupindu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.