Pata taarifa kuu

Mali yapokea ndege zisizo na rubani kutoka Uturuki

Wanajeshi walio madarakani nchini Mali wamepokea msaada wa ndege zisizo na rubani kutoka Uturuki siku ya Alhamisi wakati wa hafla mbele ya mkuu wa jeshi la serikali, Kanali Assimi Goïta, amebainisha mwandishi wa shirika la habari la AFP.

Kanali Assimi Goïta, kiongoi wa Mali, alikuwepo kwenye mapokezi ya ndege zisizo na rubani za Uturuki kwenye uwanja wa ndege wa Bamako.
Kanali Assimi Goïta, kiongoi wa Mali, alikuwepo kwenye mapokezi ya ndege zisizo na rubani za Uturuki kwenye uwanja wa ndege wa Bamako. © ORTM
Matangazo ya kibiashara

"Mamlaka za juu zaidi nchini Mali zimeelekea katika upatikanaji wa vifaa vikubwa, ikiwa ni pamoja na ndege zisizo na rubani aina ya Bayraktar TB2," amesema msimamizi wa hafla hiyo katika hotuba yake, akizungumza kwa niaba ya makao makuu ya jeshi la Mali. Ndege zisizo na rubani za Bayraktar TB2 zilizotengenezwa Uturuki zitawezesha kukagua na kufanya ulinzi nchini kote Mali, kugundua vitu viavyotiliwa shaka, kuwafuatilia na kuwapiga maadui ikiwa ni lazima kwa usahihi mkubwa, amesisitiza.

Mwandishi wa shirika la habari la AFP amehesabu ndege sita zisizo na rubani kwenye uwanja wa ndege wa Bamako. Tangu 2012, Mali imekuwa ikikumbwa na kuenea kwa wanajihadi na mgogoro mkubwa, sio tu usalama, lakini pia kisiasa na kibinadamu.

Wanajshi ambao walichukua madaraka kwa nguvu mnamo 2020 walifanya mwelekeo mpya wa kimkakati, walivunja muungano wa zamani na Ufaransa iliyotawala zamani na kugeukia kijeshi na kisiasa Urusi. Waliomba ujumbe wa Umoja wa Mataifa (Minusma) kuondoka nchini, ambao zoezi lao la kuondoka nchini humo lilikamilika Desemba 31.

Mnamo Machi 2023, walipokea ndege kadhaa kutoka Urusi na ndege zisizo na rubani kutoka Uturuki. Uwasilishaji wa vifaa vya kijeshi vya Urusi pia ulifanyika mnamo mwezi Machi na Agosti 2022 na mwezi Januari 2023.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.