Pata taarifa kuu

Mali: MINUSMA yamaliza rasmi shughuli zake, lakini hali ya usalama yaendelea kudorora

Jumapili hii, Desemba 31 inaashiria kumalizika rasmi kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali (MINUSMA), ambao ulifungaha virago mapema siku ya Jumamosi. Wakati jeshi la Mali, kwa uungwaji mkono madhubuti wa kundi la wanamgambo wa Urusi wa Wagner, liliweza kuutwaa tena mji wa Kidal kutoka kwa waasi wa muungano wa CSP-PSD mnamo Novemba 14, hali ya usalama inaendelea kuzorota: tangu siku ya Ijumaa, angalau mashambulizi mawili ya wanajihadi yalifanyika Kaskazini.

Wanajeshi wa MINUSMA kutoka Chad wakiongoza misafara kuelekea mji wa Gao, baada ya kuondoka kwenye kambi zao za Tessalit na Aguelok, kaskazini mwa Mali.
Wanajeshi wa MINUSMA kutoka Chad wakiongoza misafara kuelekea mji wa Gao, baada ya kuondoka kwenye kambi zao za Tessalit na Aguelok, kaskazini mwa Mali. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa kanda, Serge Daniel

Kuondoka kwa MINUSMA kutoka Mali si sawa na kumalizika kwa matatizo ya usalama kwenye ardhi ya Mali...angalau kwa sasa: makundi ya wanajihadi, kwa mfano, yamedai mashambulizi kaskazini mwa nchi dhidi ya ngome za jeshi la taifa.

Huko Timbuktu Jumamosi Desemba 30, makombora yalirushwa na wanajihadi. Mwezi uliopita, walirusha makombora kuelekea mji wa Kidal, ambao jeshi liliudhibiti tena mwezi uliopita. Katika taarifa kinzani, kila upande unadai kuwa umemtia hasara adui.

Kwa kundi linalodai kutetea Uislamu na Waislamu (Jnim), mshirika wa Al-Qaeda, kuondoka kwa MINUSMA na jeshi la Mali kudhibiti mji wa Kidal - kwa ushirikiano na wapiganaji wa kundi la kijeshi la Urusi la Wagner - ni hatua mpya katika mapambano. Mapambano yataendelea, amesema Iyad Ag Ghaly, kiongozi wa kundi la kigaidi, kwenye video.

Hata hivo utawala wa kijeshi nchini Mali, unasema kuondoka kwa MINUSMA badala yake ni fursa kwa jeshi la taifa kupeleka kwenye uwanja wa vita uwezo unaohitajika ili kuhakikisha usalama wa mali na watu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.