Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-USALAMA

DRC: Human Rights Watch yaonya juu hatari zinazotokana na ghasia za uchaguzi mkuu

Shirika la kimataifa la Haki za binadamu la Human Rights Watch linahofia kwamba ghasia za uchaguzi nchini DRC zitatatiza kufanyika kwa uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Desemba 20, 2023. Shirika hili la kimataifa la haki za binadamu, katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa Jumamosi, Desemba 16, lilionya kuhusu hatari zinazotokana na ghasia za uchaguzi.

Mabango ya uchaguzi mjini Kinshasa, Desemba 15, 2023.
Mabango ya uchaguzi mjini Kinshasa, Desemba 15, 2023. © Alexandra Brangeon / RFI
Matangazo ya kibiashara

HRW linabaini kuwa mamlaka ya Kongo inapaswa kuchunguza kwa haraka na bila upendeleo matukio ya vurugu yanayohusishwa na uchaguzi na kuwafungulia mashitaka waliohusika, bila kujali itikadi zao za kisiasa.

Human Rights Watch inasema imeorodhesha mapigano nchini kote kati ya wafuasi wa vyama hasimu vya kisiasa tangu mwanzoni mwa mwezi Oktoba, ambayo yamesababisha mashambulizi, unyanyasaji wa kingono na angalau kifo kimoja.

Kulingana na shirika hili, wafuasi wa chama tawala, Union for Democracy and Social Progress (UDPS), walihusika katika vitisho na mashambulizi dhidi ya viongozi wa vyama vya upinzani pamoja na wanahabari. Wafuasi wa upinzani pia walihusika katika ghasia. Matukio ya ghasia yanayohusiana na uchaguzi yanaendelea kuripotiwa.

"Mamlaka za Kongo zinapaswa kuchukua hatua za haraka ili kuzuia ghasia kabla, wakati na baada ya uchaguzia, ili kuzuia hali ambayo inaripotiwa kwa sasa isizidi," alisema Thomas Fessy, mtafiti mkuu wa Kongo katika Human Rights Watch.

"Vyama vya kisiasa na wagombea wanapaswa kuchukua msimamo wa umma kupinga ghasia na kusaidia kuhakikisha kuwa wananchi wanapata fursa ya kuwapigia kura wagombea wanaowapenda," aliongeza.

Mamlaka za Kongo zinapaswa kuhakikisha usalama wa waangalizi wote wa uchaguzi waliohamasishwa nchini humo. CENI inapaswa kuchapisha matokeo ya kura kutoka kituo cha kupigia kura baada ya kingine na kwenye tovuti ya CENI, kama inavyotakiwa kisheria, ili kuzuia uwezekano wa ghasia na unyanyasaji wa baada ya uchaguzi, Human Rights Watch iliongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.