Pata taarifa kuu

DRC: Washington yatishia kumuwekea vikwazo yeyote atakayezuia uchaguzi

Katika taarifa iliyotolewa siku ya Ijumaa, Desemba 15 na Ubalozi wake nchini DRC, Marekani inathibitisha nia yake ya kutumia vyombo vyote vilivyopo, ikiwa ni pamoja na vikwazo vya visa, ili kukuza uwajibikaji kwa mtu yeyote anayezuia uchaguzi au kudhoofisha mchakato wa kidemokrasia nchini DRC.

Wapita njia wakitembea karibu na mabango ya kampeni ya wagombea mbalimbali wa uchaguzi mkuu nchini DRC, mjini Kinshasa, Desemba 12, 2023.
Wapita njia wakitembea karibu na mabango ya kampeni ya wagombea mbalimbali wa uchaguzi mkuu nchini DRC, mjini Kinshasa, Desemba 12, 2023. © JOHN WESSELS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Dunia itqelekeza maacho yake nchini DRC katika siku zijazo huku ikifikia hatua nyingine muhimu katika historia yake.

"Tunawatakia Wakongo kila mafanikio wanapochukua fursa ya kupiga kura na kuamua mwelekeo wa mustakabali wa nchi yao," unasema ujumbe wa kidiplomasia wa Marekani.

Wakati DRC inapoingia katika awamu ya mwisho ya mzunguko wake wa nne wa uchaguzi, Marekani inawapongeza raiawa Kongo kwa kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi:

"Mwezi uliopita, tuliona watu wa nchi hii wakijaza viwanja vya michezo na viwanja vya umma kuungana na wagombea na kutoa sauti zao. Marekani inathibitisha tena kuwaunga mkono raia wa Kongo wanapotumia haki yao ya kidemokrasia kuchagua wawakilishi wao.

Washington inasema inaitegemea Serikali ya DRC kuhakikisha kwamba Wakongo wote wanaweza kushiriki katika uchaguzi huo kwa usalama na kwa njia sahihi, bila kujali utii wao wa kisiasa na bila hofu ya ghasia na kisasi.

Chanzo hicho kinawaalika wagombea wote na vyama vyote kuendeleza uchaguzi wa amani na wa kuaminika kwa kuepuka kauli zinazoweza kuchochea ongezeko na vurugu, kwa kuahidi kutatua migogoro kwa mujibu wa sheria na zaidi ya yote kwa kuheshimu matakwa ya rai wa Kongo.

Katika hatua hii ya mabadiliko katika historia ya Kongo, taarifa hiyo imesema, ni juu ya taasisi za Kongo kutimiza majukumu yao ya kikatiba kwa uhuru na uadilifu ambao rai wa Kongo wanatarajia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.