Pata taarifa kuu

DRC na Kenya zajibizana kuhusu kuzinduliwa kwa vuguvugu la kisiasa

NAIROBI – Serikali ya  DRC, imesema haikufurahishwa na hatua ya Kenya kukubali nchi yake kutumiwa na aliyekuwa kiongozi wa tume ya uchaguzi CENI, Corneille Nangaa pamoja na kiongozi wa waasi wa M23, kutangaza kuzindua vuguvugu la kisiasa linalofahamika kwa jina la Alliance Fleuve Congo, AFC. 

Corneille Nangaa, rais wa zamani wa CENI nchini DRC
Corneille Nangaa, rais wa zamani wa CENI nchini DRC AFP/Luis Tato
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa serikali Patrick Muyaya amesema haiwezekani nchi wanayoshirikiana nayo kutafuta amani, kuruhusu tukio hilo kutendeka haswa na watu amabo wako chini ya vikwazo

Katika mawazo ya pamoja mtu hawezi kuelewa kwamba nchi kama Kenya ambayo tunashirikiana pamoja katika juhudi za kutafuta amani ya Mashariki ya DRC, kwamba inaweza kukubali kufanyike shughuli mbovu za aina hiyo. 

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini DRC, Corneille Naanga akiwa jijini Nairobi Ijumaa Disemba 15, akiwa ameambatana na kiongozi wa kundi la Waasi la M 23 Betrand Bisimwa, alizindua vuguvugu hilo la kisiasa.

Vuguvugu hili limeundwa na baadhi ya vyama vya kisiasa vilivyoko nchini na nje ya nchi, mashirika ya kiraia pamoja na makundi mengine yenye silaha yanayosema kuwa yanapigania wananchi ambao wamechoka na ugumu wa maisha.

Hata hivyo serikali ya kenya imezungumzia kauli hii ya DRC kupitia msemaji wa serikali Issac Mwaura, wakati huu serikali ya Kinshasa ikimuita balozi wa Kenya nchini DRC kujieleza.

00:32

Isaac Mwaura, Msemaji wa serikali ya Kenya, Disemba 16 2023

Katika hatua nyingine, mgombea wa ubunge  Kasanga Tshomba Joseph ameauawa katika kijiji cha Makisabo na kuwaacha wengine watatu na majeraha Wilayani Beni, baada ya gari alilokuwa anasafiria kushambuliwa na waasi wanaominiwa kuwa wa ADF.

Aidha, kumeripotiwa kuuawa Sadick Espoir Ndabuye mgombea mwingine wa ubunge huko Uvira, aliyepigwa risasi Ijumaa usiku na watu wasiofahamika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.