Pata taarifa kuu

Uchumi: Ethiopia inaelekea kushindwa kulipa deni

Baada ya Zambia na Ghana, Ethiopia ni nchi ya tatu barani Afrika kukushindwa kulipa deni lake tangu mwaka 2020. Mamlaka ya Ethiopia ilitangaza kuwa nchi hiyo haiwezi kulipa deni lake la dola milioni 33 siku ya Jumatatu, Desemba 11. Hatua hiyo inaiweka Ethiopia - ambayo imeomba marekebisho ya deni - kwenye njia ya kushindwa kulipa.

Mfanyabiashara akihesabu birr (fedha) zaEthiopia kwenye duka lake katika soko la Shola huko Addis Ababa, Desemba 4, 2023.
Mfanyabiashara akihesabu birr (fedha) zaEthiopia kwenye duka lake katika soko la Shola huko Addis Ababa, Desemba 4, 2023. © Michele Spatari / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Nafasi dhaifu sana", ya akiba "chini" ya fedha za kigeni na mfumuko wa bei wa tarakimu mbili ni miongoni mwa sababu zilizoizuia Ethiopia kuheshimu malipo ya dola milioni 33 kwa wadai wake Jumatatu (Desemba 11).

Deni hili linalingana na dhamana ya kimataifa ya dola bilioni moja, ampo muda wake unamalizika mwishoni mwa 2024.

Serikali ya Ethiopia, ambayo inatafuta kurekebisha deni lake, inataka kufanya makubaliano na wamiliki wa dhamana za kibinafsi baada ya kufikia makubaliano na wakopeshaji wake wa pande mbili mwishoni mwa mwezi wa Novemba.

Ethiopia ilisimamishwa kwa muda kwa huduma yake ya deni ya euro bilioni 1.5 kwa miaka miwili - mradi tu mazungumzo na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kupata mkopo - yatakamilika ifikapo mwezi Machi 2024.

Uchumi wa nchi ya pili kwa idadi kubwa ya watu barani Afrika, ambayo hapo awali ilizingatiwa kuwa moja ya nchi zenye matumaini zaidi katika bara hilo, sasa umepungua. Imeathiriwa sana na mzozo wa Uviko-19, pamoja na atahri za vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Tigray na inaendelea kuteseka kutokana na mzozo unaoendelea katika mkoa wa Amhara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.