Pata taarifa kuu

Niger yasitisha ushirikiano wa kiusalama na ulinzi na Umoja wa Ulaya

Utawala wa kijeshi uliotokana na mapinduzi nchini Niger umetangaza siku ya Jumatatu kuwa unasitisha misheni mbili za usalama na ulinzi za Umoja wa Ulaya (EU) nchini humo.

Tangu kupinduliwa kwa rais Bazoum tarehe 26 Julai, jeshi linaloshikilia madaraka limekata uhusiano na washirika wa nchi hiyo kutoka Magharibi.
Tangu kupinduliwa kwa rais Bazoum tarehe 26 Julai, jeshi linaloshikilia madaraka limekata uhusiano na washirika wa nchi hiyo kutoka Magharibi. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Mambo ya Nje ya Niger imetangaza katika taarifa kulaani makubaliano yaliyofikiwa kati ya Niger na Umoja wa Ulaya kuhusiana na ujumbe wa kiraia wa Ulaya "EUCAP Sahel Niger", uliotumika tangu mwaka wa 2012. Ujumbe huu wenye makao yake mjini Niamey unasema kuwa una Wazungu 120 na unasaidia "vikosi vya usalama vya ndani, mamlaka ya Niger pamoja na wadau wasio wa kiserikali".

Wizara pia imetangaza "kujiondoa kwa Niger kwa idhini iliyotolewa kwa ajili ya kutumwa kwa ujumbe wa ushirikiano wa kijeshi wa EU" nchini Niger unaoitwa "EUMPM". Ujumbe huu ulizinduliwa mwezi Februari "kwa ombi la mamlaka ya Niger", "kusaidia nchi katika mapambano yake dhidi ya makundi ya kigaidi yenye silaha", kulingana na tovuti ya Baraza la moja wa Ulaya.

Niger inakabiliwa na ghasia za wanajihadi magharibi na kusini mashariki mwa nchi hiyo. Serikali ya Niger pia inaandika kwamba "inaamua kuondoa mapendeleo na kinga iliyotolewa" ndani ya mfumo wa misheni hii, bila maelezo.

Tangu kupinduliwa kwa rais mteule Mohamed Bazoum mnamo Julai 26 katika mapinduzi ya kijeshi, jeshi linaloshikilia madaraka limekata uhusiano na washirika wa nchi hiyo kutoka Magharibi. Serikali ilitaka vikosi vya Ufaransa kuondoka nchini humo- zoezi linaloendelea hadi mwisho wa mwezi wa Desemba - na inatafuta washirika wapya.

Pia siku ya Jumatatu, wajumbe wa Urusi wakiongozwa na Naibu Waziri wa Ulinzi waliwasili Niamey kujadiliana na mamlaka ya kijeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.