Pata taarifa kuu

Zambia: Wito wa uzalishaji wa chanjo barani Afrika wazidi kutolewa

Na Carol Korir, Lusaka

Mataifa ya bara Afrika yametakiwa kuchukua hatua kuelekea uzalishaji wa chanjo kwenye ardhi yake
Mataifa ya bara Afrika yametakiwa kuchukua hatua kuelekea uzalishaji wa chanjo kwenye ardhi yake © CPHIA2023
Matangazo ya kibiashara

Nchini Lusaka,wadau katika sekta ya afya wamezindua upya shinikizo za kutaka nchi za Afrika kuharakisha mchakato wa uzalishaji wa  chanjo za magonjwa tofauti yanayokabili bara Afrika. 

Shirika la udhibiti wa magonjwa katika Ukanda wa Afrika,CDC,kwa ushirikiano wa shirika la pamoja la usambazaji chanjo,GAVI, limeahidi ufadhili wa Dola Bilioni moja kuzisaidia kampuni za Afrika  zinazojikita kwenye uzalishaji wa chanjo. 

Ufadhili huo wa 1bn unatazamiwa kuthibitishwa na bodi ya CDC mwezi Disemba katika kikao cha bodi ya usimamizi .

Dr Jean Kaseya ni mkurugenzi  mkuu wa CDC ukanda wa Afrika. 

“Nirudie kusema uzalishaji wa chanjo hapa barani ni ukombozi wa pili wa Afrika, Tuliona wakati wa uviko 19 kwamba mabara mengine yanaweza kufunga milango na tukabaki wenyewe,mliona jinsi watu wetu wanaweza kupoteza maisha wakikosa chanjo sahihi,nani atakubali hili? Tunaendelea na mchakato wa kuhakikisha mfumo mmoja wa ununuzi ili kuhakikisha kuwa chanjo au dawa zinazotengenezwa Afrika zinatumika kwanza,tutatumia ubaguzi ila kwa njia chanya kuhakikisha bidhaa zetu zinatumika kwanza”. 

Rais wa Zambia Hakainde Hichelema kwa upande wake amesisitiza umuhimu wa nchi za Afrika kushirikiana ili kusiwe na mataifa mengi yanayozalisha aina mmoja ya chanjo bila kuwepo kwa soko la chanjo hizo. 

Amesisitiza aidha nchi zinazopanga kutengeneza chanjo hapa barani kuzingatia ubora wa juu na kufanya biashara na mataifa mengine ya Afrika kwa njia ya haki. 

"Afrika lazime iende sambamba na nchi zingine hata katika uzalishaji wa chanjo,na tutakapoanza uzalishaji ,lazima tuzingatie ubora ambao upo Katika maeneo mengine,tunachosema ni tushirikiane  n anchi zinazotengeneza chanjo tayari ila tulipia gharama ya haki ,njooni muwekeza kwetu ,leteni mtaji ila kwa gharama isiyo juu sana." alisema rais wa Zambia. 

Shirika la afya duniani ,WHO ,mapema mwaka huu ,lilizundua ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha chanjo ya Uviko 19 kutumia teknoljia ya MRNA,mradi huu ukilenga kuzisaidia nchi zinazoendelea. 

Kenya pia ni nchi nyingine ambayo WHO imeidhinisha mradi kama huo kuendelea. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.