Pata taarifa kuu

Zambia: Kesi dhidi ya Esther Lungu imeanza kusikilizwa

Kesi dhidi ya Esther Lungu, aliyekuwa mke wa rais wa zamani wa Zambia Edgar Lungu, imeanza mjini Lusaka.

Kesi dhidi ya Esther Lungu, mke wa aliyekuwa rais wa Zambia Edgar Lungu imeanza
Kesi dhidi ya Esther Lungu, mke wa aliyekuwa rais wa Zambia Edgar Lungu imeanza © Edgar Lungu- X
Matangazo ya kibiashara

Esther Lungu ameshtakiwa kwa wizi wa magari matatu, wizi wa hatimiliki ya mali huko Lusaka pamoja na kupatikana na $400,000 (£317,000) zinazodaiwa kupatikana kwa njia za kihalifu.

Aidha ameshtakiwa pamoja na maafisa wawili wa polisi.

Mmoja wa mashahidi aliiambia mahakama siku ya Jumatatu kwamba Esther Lungu alichukua kwa nguvu gari lake na hati miliki ya nyumba yake pamoja na magari mawili ya bintiye.

Aliongeza kuwa maafisa wa polisi walioshtakiwa waliwalazimisha kutia saini hati za mali hizo kwa mke wa Lungu.

Washtakiwa walikanusha makosa hayo  walipokamatwa kwa madai ya mwezi Septemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.