Pata taarifa kuu

Viongozi wa Afrika kuipa kipau mbele huduma za afya wakati wa mizozo na majanga

Na Carol Korir, Lusaka

Kongamano kuhusu afya barani Afrika linafanyika nchini Zambia
Kongamano kuhusu afya barani Afrika linafanyika nchini Zambia © Hakainde Hichilema
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa Afrika kwa ushirikiano ya mashirika ya kikanda yanayoangazia afya wamekutana jijini Zambia kwa kongamano la tatu kuhusu afya ya umma ,wito ukitolewa kwa nchi za Sahel kuzingatia utoaji wa huduma za afya licha ya kuathirika na mizozo tofauti. 

Kikao hicho kinachoratibiwa na Umoja wa mataifa kwa ushirikiano na shirika la udhibiti magonjwa barani Afrika ,CDC ni muendelezo wa mjadala kuhusu mfumo wa afya barani baada ya janga la Uviko 19. 

Dr Jean Kaseya mkurugenzi wa shiriki la udhibiti wa magonjwa barani Afrika CDC amesisitiza umuhimu wa mataifa ya Afrika ambayo kwa sasa yanashuhudia ongezeko la mizozo ya kisiasa na utovu wa usalama kukumbatia diplomasia katika sekta ya Afya. 

Amesema CDC imeanza mkakati kuwasaidia nchi za ukanda wa Sahel ambazo hivi karibuni imekubwa na msururu wa  mapinduzi ya kijeshi kukabiliana na hali za dharura katika huduma za afya na mlipuko wa magonjwa hatari. 

"Tunahitaji kuwa na uthabiti katika swala la diplomasia katika afya,hata kama unapigana kisiasa,au hata kijeshi,kukiwa na mlipuko wa ugonjwa ,unavunja mipaka bila kujali. Haijalishi ni wakati gani tunastahili kupambana na mlipuko,tunasaidia nchi za Afrika Magharibi kukabiliana na dharura pamoja na nchi zingine." alisema Dkt Kaseya katika ufunguzi wa kongamano la CPHIA katika chumba cha mkutano cha Kennedy Kaunda. 

00:31

Dr Jean Kaseya kutoka Africa CDC

Rais wa Zambia Hakainde Hichelema akifungua rasmi kikao hicho,amesistiza nguvu ya uongozi katika kufanikishwa sera za afya. 

Kwa mujibu wa rais Hakainde, bara Afrika kando na kuhitaji nia ya kisiasa inahitaji pia kutambua nafasi ya kuwa mpambanaji. 

"Naweza kukudhirishia kuwa katika AU kama viongozi wa Afrika tumejitolea kuhakikishia kuwa tunapata huduma bora za afya,wanapopata wengine." alisisitiza rais Hichelema. 

00:14

Rais wa Zambia kuhusu CPHIA

Naye mwenyekiti wa waandaji wa kongamano la CPHIA Profesa Magret Gyapong amesisitiza ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi kupambana na magonjwa yaliyochangamoto kwa Afrika. 

"Ushirikiano kati ya serikali na sekta ya binafsi pia mashirika ya kiraia, kubadilishana ufahamu na kuweka pamoja rasli mali ,umeboresha ukuaji wa teknolijia katika afya ya umma. Ufanisi kwenye chanjo ya malaria ya RTS ni dhihirsho tosha ya ushirikiano wa wanasayansi wa Afrika pamoja na washirika muhimu  kukabilia matatizo ya afya ya Afrika. "alisema profesa Magret. 

Idadi ya mataifa ya Afrika yanayoshuhudia mizozo imezidi kuongezeka kuanzia ukanda wa Sahel,Afrika ya kati na hata Pembe ya Afrika. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.