Pata taarifa kuu

Somalia: Idadi ya waliofariki kutokana na mafuriko  inakaribia watu  100

Nairobi – Idadi ya waliofariki kutokana na mafuriko nchini Somalia inakaribia 100, huku takriban watu milioni mbili wakiathirika, baraza la mawaziri la nchi hiyo limesema siku ya Alhamis ya wiki hii.

Zaidi ya watu laki 1 na elfu 13, wamepoteza makazi yao kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunysha nchini humo
Zaidi ya watu laki 1 na elfu 13, wamepoteza makazi yao kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunysha nchini humo REUTERS - FEISAL OMAR
Matangazo ya kibiashara

Somalia, kama nchi nyingine katika Pembe ya Afrika, inakabiliwa na mvua kubwa na mafuriko, wakati huu ikiwa imetoka kushuhudia hali mbaya kutokana na ukame uliowaweka mamilioni ya raia kwenye hatari ya kufa kutokana na baa la njaa.

Serikali mapema mwezi huu, ilitangaza hali ya hatari kutokana na mafuriko, ambayo yamesababisha watu zaidi ya laki 7 kupoteza makazi, mashamba na miundombinu mingine.

Somalia ni mojawapo ya mataifa yalioathirika na mafuriko
Somalia ni mojawapo ya mataifa yalioathirika na mafuriko REUTERS - FEISAL OMAR

Mvua zinazoendelea kunyesha nchini humo zinahusishwa na hali ya hewa ya El Nino, ambayo inatarajiwa kudumu hadi angalau mwezi April mwakani.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kutoa misaada ya kibinadamu OCHA, mamia ya watu wamefariki pia katika nchi za Ethiopia na Kenya, mashirika ya misaada yakionya kuwa huenda hali ikawa mbaya zaidi.

Kaunti ya Mombasa nchini Kenya ni mojawapo ya maeneo yalioathirika zaidi ya mafuriko yanayotokana na mvua inayoendelea kunyesha kwenye taifa hilo
Kaunti ya Mombasa nchini Kenya ni mojawapo ya maeneo yalioathirika zaidi ya mafuriko yanayotokana na mvua inayoendelea kunyesha kwenye taifa hilo REUTERS - STRINGER

Watu wanaokadiriwa kufikia 75, wameuawa katika kipindi cha wiki mbili zilizopita kutokana na vurugu kati ya jamii mbili hasimu kwenye eneo lenye mgogoro la Abyei, katika mpaka kati ya nchi ya Sudan Kusini na Sudan, amesema mwakili wa katibu mkuu wa UN kwenye nchi ya Sudan Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.