Pata taarifa kuu

Marekani kurejelea utoaji wa misaada nchini Ethiopia mwezi Desemba

Marekani imesema itarejelea tena mpango wake wa usambazaji wa chakula cha msaada katika baadhi ya maeneo nchini Ethiopia mwezi Desemba mwaka huu.

Marekani imeeleza kuwa mpango huo utafanyiwa majaribio ya mwaka moja kuona iwapo mageuzi yametekelezwa kama inavyohitajika
Marekani imeeleza kuwa mpango huo utafanyiwa majaribio ya mwaka moja kuona iwapo mageuzi yametekelezwa kama inavyohitajika Getty Images - J. Countess
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hili Washington linakuja ikiwa imepita miezi sita baada ya kutangaza kusisitishwa kwa mpango huo kutokana na madai ya wizi wa chakula hicho pamoja na kuhusishwa maofisa kwenye taifa hilo na ufisadi.

Shirika la misaada la Marekano (USAID) limesema mageuzi makubwa yanahitajika kufanywa ilikuruhusu misaada hiyo kuwafikia walengwa na kuzuia kuelekezwa kwengine.

Mashirika ya misaada ya umoja wa mataifa na Marekani yamekuwa yakitoa msaada wa wathiriwa wa ukame na njaa nchini Ethiopia
Mashirika ya misaada ya umoja wa mataifa na Marekani yamekuwa yakitoa msaada wa wathiriwa wa ukame na njaa nchini Ethiopia © via REUTERS - WORLD FOOD PROGRAMME

Aidha Marekani imeeleza kuwa mpango huo utafanyiwa majaribio ya mwaka moja kuona iwapo mageuzi yametekelezwa kama inavyohitajika.

Mamilioni ya raia wa Ethiopia wanakabiliwa na uhaba wa chakula kutokana na mizozo inayoendelea kwenye taifa hilo pamoja na mabiliko ya hali ya hewa, ukame wa muda mrefu pia ukiwa umeathiri sehemu kubwa ya raia.

Ukame wa muda mrefu katika pembe ya Afrika umeripotiwa kuchangia pakubwa ongezeko la watu wanaohitaji misaada
Ukame wa muda mrefu katika pembe ya Afrika umeripotiwa kuchangia pakubwa ongezeko la watu wanaohitaji misaada AP - Ben Curtis

Mpango huo ulisitishwa mwezi Juni kutokana na malalamishi ya kutoka kwa raia kuhusu baadhi ya maofisa wa serikali kuelekeza misaada hiyo kwengine.

Ulirejelewa kwenye kambi za wakimbizi mwezi uliopita ila sio kwa sehemu kubwa kama ilivyokuwa hapo awali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.