Pata taarifa kuu

Utawala wa kijeshi wa Mali wakanusha shutuma za HRW dhidi ya jeshi lake

Utawala wa kijeshi unaoshikilia madaraka nchini Mali umesema hitimisho la ripoti ya hivi majuzi la shirika lisilo la kiserikali la Human Rights Watch (HRW) linalowatuhumu wanajeshi wake na wanaodaiwa kuwa wanachama wa kundi la Wagner kuwaua raia 40 katika operesheni, halina msingi wowote, na ni uwongo mtupu.

"Vikosi vya Wanajeshi wa Mali vinatekeleza jukumu lao kwa kuheshimu sana haki za binadamu na sheria za kimataifa za kibinadamu," inajibu Wizara ya Mambo ya Nje ya Mali.
"Vikosi vya Wanajeshi wa Mali vinatekeleza jukumu lao kwa kuheshimu sana haki za binadamu na sheria za kimataifa za kibinadamu," inajibu Wizara ya Mambo ya Nje ya Mali. © REUTERS/Benoit Tessier
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Mambo ya Nje ya Mali inashutumu "mtazamo unaoegemea" wa ripoti ambayo "inaliweka jeshi la Mali katika ngazi sawa na makundi ya Kiislamu yenye silaha", katika jibu lililotumwa kwa waandishi wa habari siku ya Jumatatu. Utawa wa kijeshi wa Mali unakosoa "madai yasiyo na msingi, madai ya upendeleo na hitimisho potofu". Unakanusha tena ushirikiano wowote na kundi la wanamgambo wa Urusi Wagner, bila kutaja jina hilo. Kwa mara nyingine tena unataja ushirikiano wa zamani wa nchi kwa nchi kati ya Mali na Urusi.

Wanajeshi waliochukua kwa nguvu mnamo mwezi Agosti 2020 madaraka ya uongozi wa nchi hii inayokabiliwa na mashambulizi ya wamgambo wa kijihadi na mzozo wa pande nyingi ulivunja ushirikiano wa kihistoria wa kijeshi na Ufaransa mnamo 2022 na kugeukia kisiasa na kijeshi Urusi. Waangalizi wengi wameripoti uwepo wa wanamgambo wa kindi la Wagner nchini Mali tangu mwisho wa mwaka 2021.

HRW ilichapisha wiki iliyopita mahitimisho ya uchunguzi wake katika operesheni tano zilizofanywa kati ya mwezi Aprili na mwezi Septemba nchini Mali, ama na wanajihadi au na jeshi. Kundi la linalodai kutetea Uislamu na Waislamu (GSIM), muungano wa wanajihadi wenye mafungamano na Al-Qaeda, wanahusika na vifo vya takriban raia 135 katika mashambulizi mawili, linasema shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Human Right Watch. Wanajeshi wa Mali na wanamgambo wanaoaminika kuwa wa kundi la Wagner waliwaua raia 40 katika operesheni tatu, limesema shirika hilo, kulingana na shuhuda zilizokusanywa kwa mbali.

"Vikosi vya Wanajeshi wa Mali vinatekeleza jukumu lao kwa kuheshimu sana haki za binadamu na sheria za kimataifa za kibinadamu," inajibu Wizara ya Mambo ya Nje ya Mali.

Wizara hiyo inahakikisha kwamba hakuna dhuluma yoyote iliyotajwa na HRW iliyoripotiwa kwa mamlaka na kwamba moja ya operesheni iliyotajwa ililenga makundi ya wanamgambo wa kijihadi, bila athari kwa raia. Wizara inakariri kuwa ripoti zote za ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu zinachunguzwa na kwamba baadhi ya wanajeshi tayari wamehukumiwa. 

Wizara ya Mali pia inakosoa mbinu ya HRW, hasa ukweli wa kuwahoji mashahidi kwa mbali. Upatikanaji wa maeneo na mashahidi husika ni mgumu sana kwa sababu mbalimbali, hasa usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.