Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Mali: Wagner yanyooshewa kidole cha lawama kwa 'ukatili mpya'

Siku kumi baada ya kuchapisha ripoti kuhusu ghasia zinazofanywa na makundi ya wanajihadi nchini Mali, shirika la kimataifa la haki za binadamu safari hii limeorodhesha kesi mpya za unyanyasaji unaofanywa na jeshi la Mali na wasaidizi wake wa Urusi. Human Rights Watch inatoa wito kwa Umoja wa Afrika na ECOWAS kulaani ukatili huo na kuchukuwa hatua.

Gari la jeshi la Mali huko Timbuktu, Septemba 9, 2021.
Gari la jeshi la Mali huko Timbuktu, Septemba 9, 2021. AFP - MAIMOUNA MORO
Matangazo ya kibiashara

Ouenkoro, Séguéla, Sossobé… Human Rights Watch ilikusanya ushuhuda wa takriban mashahidi ishirini wa moja kwa moja, lakini pia wa familia za waathiriwa, wawakilishi wa jamii na wajumbe wa mashirika ya kiraia, kutoka Mali na wale wa mashirika yasiyokuwa ya serikali kutoka nchi za kigeni.

Operesheni zilizofanyika mwezi Februari na Machi mwaka jana katika vijiji hivi katika mikoa ya Mopti na Ségou, katikati mwa Mali, zinawakilisha, kulingana na Human Rights Watch, "sehemu tu ya unyanyasaji unaofanywa" na jeshi la Mali na wasaidizi wake wa Urusi, lakini shirika hili limekusanya shuhuda nyingi na sanjari kwa kesi hizi.

Vurugu na uporaji

Wanakijiji wa Séguéla wanataja uvamizi wa "dazeni za wapiganaji wazungu waliovalia sare za kijeshi". Huko Sossobé, wanajeshi wa Mali waliwasili na wasaidizi wao wa Urusi wakitumia helikopta, huko Ouenkoro pia, siku ya soko. Mashahidi wanasimulia matukio ya ufyatuaji risasi kiholela kutoka kwa helikopta, kuwakusanya wanaume mbele ya msikiti wa kijiji, uharibifu na misako ya nyumba kwa nyumba iliyoambatana na vurugu na uporaji ulioambatana na wizi wa fedha au vito.

Iwapo wanajihadi wa JNIM (Kundi llinalotetea Uislamu na Waislamu), wanaohusishwa na al-Qaeda, wanafanya endesha harakati zao katika maeneo haya, Human Rights Watch inalaani "mauaji" na "visa vya watu kadhaa kutoweka, na vile vile vitendo vya "mateso" vinavyofanywa ndani ya mfumo wa operesheni inayopambana na ugaidi, dhidi ya watu kutoka jamii ya Fulani, kulingana na Human Right Watch

Uchunguzi wafunguliwa

Human Right Watch inatoa wito kwa Umoja wa Afrika na Jumuiya ya kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, ikizitaka "kuongeza shinikizo kwa mamlaka ya Mali [...] ili kukomesha [...] unyanyasaji mkubwa unaofanywa na vikosi vya jeshi vya Mali na wapiganaji wanaodaiwa kuwa na uhusiano na kundi la Wagner".

Katika kujibu ripoti hii ya Human Rights Watch, serikali ya mpito ya Mali inashutumu uchunguzi unaolenga "kupaka tope" jeshi la Mali, na hivyo kukanusha kulengwa kwa kabila la Fulani na kuani kwamba mbinu iliyotumiwa na shirika hili kwa kufanya uchguzi wake "haiaminiki". Bamako inabainisha kuwa "katika kipindi husika, serikali ya Mali haikufahamu kuhusu kesi yoyote ya ukiukaji wa haki za binadamu iliyofanywa na jeshi la Mali, FAMA, " lakini kwamba, kufuatia madai yaliyomo katika ripoti hii, uchunguzi wa "uhalifu wa kivita" na "uhalifu dhidi ya binadamu" utafunguliwa na vyombo vya sheria vya Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.