Pata taarifa kuu

Ujerumani na Mali zakubaliana kuhusu kuanza kuondoa wanajeshi wa Berlin jijini Bamako

Nairobi – Ujerumani na Mali, zimekubaliana kuwa na utaratibu mzuri wa utawala wa Berlin kuanza kuondoa wanajeshi Wake nchini humo, makubaliano yaliyofikiwa majuma kadhaa kupita tangu umoja wa Mataifa uridhie kuhitimishwa kwa operesheni zake kwenye taifa hilo.

Hatua ya Ujerumani inakuja miezi kadhaa kupita baada ya Ufaransa kuwaondoa wanajeshi wake katika operesheni Barkhane
Hatua ya Ujerumani inakuja miezi kadhaa kupita baada ya Ufaransa kuwaondoa wanajeshi wake katika operesheni Barkhane © MINUSMA (UN)
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Waziri wa Ulinzi wa Mali Kanali Sadio Camara, aliihakikishia Berlin kuwa serikali yake inaunga mkono mpango huo utaratibu ambao pia umeidhinishwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa Minusma ifikapo mwisho wa 2023.

Wizara ya Ulinzi ya Ujerumani iliithibitisha taarifa hii hapo jana na kwamba baada ya mawasiliano wa mawaziri wa ulinzi wa Mali na Ujerumani Boris Pistorius, zoezi hili halitachukua muda.

Hatua ya Ujerumani inakuja miezi kadhaa kupita baada ya Ufaransa kuwaondoa wanajeshi wake katika operesheni Barkhane, wadadisi wa mambo ya usalama wanadai hali hii huenda ni kutokana na ushawishi wa kikosi cha mamluki kutoka Urusi cha Wagner.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.